Mangwasha yuko na wanawe Sayore na Kajewa ndani ya kanisa fulani. Walikimbilia huku kutoka kwao Matango baada ya kuchomewa nyumba zao, yeye na Waketwa wenzake. Palikuwepo fununu zilizosema kwamba palikuwa watu fulani waliotaka kuitwaa ardhi yao Matango kwa nguvu. Zaidi ya hayo, ni wazi kwamba, katika mji wa Taria, jamii ya Waketwa na ile ya Wakule zilikuwa mahasimu wa tangu jadi. Kiongozi wa nchi ya Matuo, Mtemi Lesulia anatoka katika jamii ya Wakule na anawachukia watu wa jamii ya Waketwa.
Mangwasha anafanya kazi ya uhazili katika afisi ya Chifu Mshabaha. Ana ufahamu tosha kwamba Chifu Mshabaha hawapendi Waketwa na kwamba anafanya mpango wa kuwadhulumu. Hili linamsukuma Mangwasha kutaka kuzungumza na kiongozi wao, Lonare ili amjulishe yale yanayopangwa na akina Mshabaha.
Lonare, kiongozi wa Waketwa ni mtu maarufu kote nchini na katika uchaguzi wa awali, alitokea kuwa na sera bora ikilinganishwa na mpinzani wake. Hata hivyo, hakupata kuchaguliwa kwani alitekwa nyara kabla ya uchaguzi kufanyika na hivyo basi, Mtemi Lesulia akachaguliwa bila kupingwa. Tunaarifiwa kwamba Lonare alipangiwa njama nyingi za kumwangamiza lakini alifaulu kuepuka mitego yote hiyo kutokana na busara yake. Alikiuwa na ruwaza njema ya kusaidia nchi yake na kuibadili. Mashambulizi yanapotekelezwa dhidi ya Waketwa, Mangwasha anamwona Lonare kama nafuu ya pekee kwa Waketwa na njia mwafaka ya kuwajulisha watu wao yale yaliyokuwa yakipangwa dhidi yao.
Juhudi za Mangwasha, hata hivyo, zinatatizwa na hali kwamba jamii haimthamini mwanamke, na anashangaa kama atasikilizwa. Anaamua atafanya tu alilokusudia, liwe liwalo.
- Uhasama wa kijamii/kikabila kati ya Wakule na Waketwa ambapo Waketwa wamechomewa nyuma zao na Wakule kutokana na chuki na uhasama wa tangu jadi. Uhasama huu pia unawafanya Waketwa kunyang’anywa ardhi yao. Zaidi ya hayo, Waketwa wanaluamiwa kwa kila janga katika nchi ya Matuo, mvua ya mafuriko iliponyesha na kusomba watu, waketwa walilaumiwa. Maradhi yakitokea, wa kulaumiwa ni Waketwa. Kila jambo lililoshindikana lilisemekana kusababishwa na Waketwa.
- Mrima kuitelekeza familia yao na kupotelea sikokujua mkewe.
- Umaskini. Tunamwona Mangwasha akiwa amekabiliwa na umaskini mkubwa. Hali hii inadhihirika kutokana na vyombo na bidhaa zake za nyumbani. Tunaambiwa kwamba: …alivitazama vitu vilivyokuwa mbele yake. Akali tu ya vitu. Hiindiyo iliyokuwa milki yake na wanawe.
- Pia pana swala la utabaka. Tunapta kuona kwamba, watu wa tabaka la juu, wengi wao wakiwa Wakule, waliishi katika mtaa wa Majuu.
- Swala la ukabila pia linajitokeza. Hapa Waketwa wanbaguliwa kiwango kwamba wananyimwa ajira kwa misingi ya majina au kabila lao.
- Mfumo wa ubabedume unawanyima wanawake nafasi ya kujiamini kama wahusika sawa katika jamii. Mwanamke asiyekuwa na cheo au pesa hawezi kusikilizwa.
Kilimani, Nairobi, Kenya
info@kwiksaf.com
+2547974180990
© Kwik Saf. All Rights Reserved. Designed by Kwik Saf Express