Hii ni sehemu yetu ya pili ya Mwongozo Bembea ya Maisha. Unaweza kusoma sehemu ya kwanza hapa: Sehemu ya kwanza.

Previous <<Sehemu ya Kwanza

SEHEMU YA PILI

Bembea-ya-maisha
Bembea Ya Maisha


ONYESHO I


Onyesho hili linatokea mjini katika nyumba ya Neema. Neema na Sara wako mazungumzoni baada ya kufika kutoka kijijini. Wawili hawa wanaongea kuhusu hali ya anga iliyo na joto sana. Sara analalamikia hali uchofu wa safari na kuajabia kuwa, akina Neema huendesha magari yao kwa muda mrefu. Analalamika pia kwamba wamekuwa wakiahidiwa maendeleo tangu utotoni mwao lakini maendeleo hayo hayaji. Anaona kwamba hayatafika katika kipindi cha uhai wao. Anasema kwamba, wamepewa ahadi tupu na wanasiasa wanaotumia lugha tamu ya misemo na ahadi.

Kutokana na mazungumzo ya Neema na Bela, mfanyakazi wake wa nyumbani, twafahamu kuwa Neema ana motto aliye shuleni. Mtoto huyu amechelewa kufika kwa kuwa ni siku ya mazoezi. Neema alalamika kuwa mambo ni mengi kwa vile hapati hata wasaa wa kuwa na mwanawe. Sara anamwambia kuwa mambo yalikuwa mengi tangu zamani. Anamhimiza Neema kwa kumwambia kuwa mrina haogopi nyuki. Anaendelea kumhimiza Neema asikate tama na kumwambia kuwa ana uhakika hakuingia katika bahari isiyokuwa yake. Anamwambia kuwa libasi ya mkulima hodari huwa imechakaa ikilinganishwa na ya mkulima wa nguo safi. Anamweleza Neema kuwa ako na bahati kupata watoto ujanani mwake kinyume naye aliyechelewa kujaliwa watoto. Anamwomba awalee vyema na shukuru Mungu kwa sababu yao.

Neema anashangaa Sara amwambiapo kuwa hata Yona alifurahi walipojaliwa watoto. Anashangaa mbona basi akawatenda aliyowatenda: kugombana na kulalamika. Sara anamwambia kwamba hilo ni jambo la kawaida kwa wanadamu. Anaeleza kuwa, Yona alishinikizwa na watu pale alipokosa mwana wa kiume ndiposa akawa mkali kwa familia yake na mwishowe kukumbatia ulevi. Hili pia lilimfanya aitelekeze kazi yake na akaishia kusimamishwa kazi ya ualimu. Sara alimvumilia Yona kwa yote na sasa wanataniana kuhusu jambo hilo ambalo lilikuwa karibu kuwaponza roho.

Tunafahamu kutoka kwa Neema kwamba, daktari alisema ugonjwa wa Sara ulisababishwa na vurumai na matusi kutoka kwa Yona. Kwa Sara, hili si jambo la ajabu, anasema kuwa hivyo ndivyo ilivyoandikwa na kwamba, kama haneupata ugonjwa huu, angepatwa na mwingine. Anamwabia Neema asidadisi zaidi wala asitake kujua nyuki ametumia nini kuandaa asali. Anayalinganisha masiha na vidole, havifanani. Pia anayalinganisha maisha na watoto wachezao bembea; kila mmoja hucheza wakati wake.

Sasa ni wakati wao na haijalishi kama bembea ni ya chuma au kamba. Muhimu ni kwamba wameshirkiana kusukumana kwenye bembea yao ya maisha. Kunao wakati inakuwa na raha na wakati mwingine hukatika na kubwaga watu. Anasema kuwa hiyo ndiyo raha ya maisha, sawa na chombo kinachomenyana na mawimbi baharini. Mawimbi yajapo, watu husahau mema ya awali. Anaendelea kusema kuwa, bembea ikatikapo, hiyo haiwi mwisho wa mchezo bali huungwa na mchezo kuanza tena. Sara anasema ameridhia Yona kwani ndiye aliyepewa. Neema anashangaa jinsi Sara amteteavyo ‘mlevi wake’ na kusema, “Ama kweli mwana wa yungi hulewa….” Onyesho linaishia kwa Neema kusema: Kipenda roho hula nyamba mbichi akirejelea mapenzi ya Sara kwa Yona.

ONYESHO II

Advertisement


Onyesho hili latokea nyumbani kwa Neema siku mbili baada ya mazungumzo kati ya Neema na Sara. Hapa patokea mazungumzo baina ya Bela na Neema. Bela ni mfanyakazi wa nyumbani wa Neema. Wanazungumzia hali ya maisha na vile kila mmoja maishani anatoa sauti ya kilio. Neema anasema kuwa maisha ya sasa hayana fundi. Yanamwendesha kila mtu kama tawi linalosukumwa hadi kung’oka kutoka tagaani na kupeperushwa na upepo.


Mara, wawili hawa wanageukia swala la motto wa Neema ambaye yadhihirika kuwa walikuwa na michezo na nyimbo shuleni mwao. Tayari sasa ashalala. Imekuwa desturi kwamba Neema atokapo kazini hupata Lemi(mwanawe) akiwa amelala na aondokapo kwenda kazini Lemi huwa bado usingizini. Neema analinganisha maisha ya kazi na safari ya ahera ambayo hakuan aliye na habari nayo. Ni kama gurudumu kwenye gari la masafa marefu ambalo huviringishwa bila lenyewe kupenda. Analinganisha maisha ya mfanyakazi na tiara ambayo hupeperushwa na upepo huku mshika tiara ardhini akiwa anaona raha tu. Bela anakubaliana naye na kusema kuwa, mtu asipoyumbishwa namna hiyo, atakaa mjinga. Hataweza kufikiri. Anaongeza kuwa adha ndiyo chanzo cha uvumbizi.


Neema anasikitika kuwa hawaonani na mwanawe. Humwona tu usingizini wala hasemi naye, hali naye wala kucheza naye. Anaushangaa uzazi wa aina hii. Bela anamwambia asijali kwani hata yeye hakuwaona wanawe hadi ukubwani kutokana na hali za kikazi. Neema naye analinganishwa watu wa mapato ya chini na miti michanga katika chaka la miti mirefu. Hawa hutapia hewa na jua na kutoa shingo zao kung’ang’ania mwanga. Neema ansema kuwa, msongamano barabarani unachangia pia kuchelewa kwa wazazi kufika nyumbani na kuonana na wanao.
Kwingineko, Bela anamdadisi Neema alikokwenda Sara. Anashangaa kwa nini hawezi kuka pale kwa Neema. Neema anamweleza kuwa alimpeleka kwa Asna, dadake Neema. Anamwambia kuwa, desturi yao haimruhusu Sara kulala pale. Bela anapuuza desturi hii kwa kusema kuwa hayo ni mambo ya kale na kuwa ya kale hayanuki.

ONYESHO III


Mapema asubuhi nyumbani kwa Neema baada ya siku mbili. Neema na mumewe kwa jina Bunju wako sebuleni wanaongea. Bunju anashangaa ni kwa nini Lemi hajaamka naye Neema anasema kuwa bado ni mapema. Bunju anasema ni vyema azoee kuamka mapema. Anasema mapema ina sudi na akichelewa atakuta wenziwe wameenda nayo. Anasisitiza ujumbe huu wake kwa methali kuwa, afikaye kisimani mapema hunywa maji maenge. Kulingana naye, Lemi apaswa kufundishwa tangia utotoni kurauka mapema. Anamlaumu Neema kwa kumdekeza na anamwambia kuwa samaki hukunjwa angali mbichi.

Neema anasema hamdekezi mwana. Swala la masomo ya Lemi linazuka pia. Neema anasema alama za Lemi zimepanda lakini nafasi darasani inashuka. Jambo hili linamuudhi Bunju anayesema kuwa, afadhali apunguze alama lakini nafasi yake darasani ipande. Kwa Neema, alama ndizo bora kuliko nafasi ila kwa Bunju ni kinyume chake.


Neema anaiona hali ya mwanao kama majaliwa lakini BUnju hataki kusikia hilo.
Neema anamweleza Bunju kuhusu hali ya Sara, mamake Neema na jinsi alivyo mgonjwa. Bunju anasema hawezi kusaidia kwa lolote kutokana na majukumu yake mengi. Anasema ana mkopo wa benki wa kujenga nyumba yao hii. Vile vile anasema Neema alikazania mwanao Mina aendes sule ya ‘boarding’ tena ya gharama kubwa. Neema anaona ni vyema motto wa kwanza kusomea shule iliyo na matumaini. Bunju anatoa kauli kuwa ametekeleza wajibu wake kwa familia yake; kununua chakula na mavazi. Vile vile amemnunulia Neema gari. Anamwambia Neema kuwa ni mchache wa fadhila.

Mzigo wa Bunju unamtosha na kwamba haliwezi lingine. Anahesabu yote aliyoyafanya. Kwanza amemwachia Neema kuutmia mshahara wake kuinua familia yake, amemsomesha Salome shule ya upili na chuo kikuu na amekuwa akiishi pale pamoja nao. Anamwambia mkewe kuwa ana bahati na sio kama wale wanawake wasiokuwa na kazi. Tena, anaelewa changamoto za walio na mishahara: mara kitita kikubwa cha pesa lakini mahitaji mengi yanakuacha kama asiye na pesa. Anamsisitizia Neema pia kuhusu desturi yao ambayo hamruhusu kukaa na wazazi wa Neema katika nyumba moja.

Anasema pia kwamba, hata wazazi wake mwenyewe walipokuwa hai hawakuwahi kuja kuishi kwake. Kwa hili Neema ana sema ni kwa kuwa yeye ni kitindamimba na kwamba safari za wazazi wake ziliishia kwa wakubwa wake lakini Neema ndiye mkubwa kwao.
Kutokana na mazungumzo haya, ni wazi kwamba Bunju anashikilia kukutu desturi na mila za kwao na hayuoka tayari kuubadili msimamo wake. Neema naye anaomba kusikizwa ka kusaidiwa na mumewe.


Kwa maneno yake Neema kwa hadhira, maisha ya ndoa anayalinganisha na abiria katika gari liendalo kasi. Mtu hutamani dereva apunguze mwendo lakini pia safari ni ndefu na hutaki kuchelewa. Mtu anatamani kushuka lakini huwezi kwani safari itaganda. Inabidi mtu atulie ndani japo unajikuta umetambaliwa na uchovu, shaka na tuhuma.


Neema anasema kuwa mumewe amejitahidi japo hana uhakika kwamba anamwelewa Neema. Kwa Neema, Sara ni mboni ya jicho kwake na kwa wanuna wake. Anasema kuwa, mama anamhitaji katika kipindi hiki cha lala salama; maanake, siku zake za uzeeni, mkondo wake wa mwisho wa maisha duniani. Neema anaapa kwamba hatamsaliti mamake kwa sababu ya ugumu wa maisha.


Lemi anajiunga na mamake na kuomba kujua kana kwamba kunaye mtu aliyemkasirisha au kumkosea mamake. Neema ansingizia hali yake ya huzuni kwa shughuli za kazini mwake. Hapa tunakuja kujua kwamba, yeye hufanya kazi katika kampuni ya uuzaji wa kompyuta.

ONYESHO IV

Onyesho hili linafanyika asubuhi na mapema nyumbani kwake Asna-chumba kidogo katika mtaa wa kifahari. Asna wako na Sara ambapo Sara analalmikia maisha ya mjini akisema yamejaa adha. Asna anayalinganisha na maisha ya kijini na kyuaona bora kwa kuwa, kulingana naye, kijijini ndikokuliko na umaskini weneyewe. Anasema kwamba hawezi kurudi kijijini na elimu yote aliyopata. Sara anamrai kwa kumwambia kuwa: maskini mtu kwao, ugeni si kitu chema. Anamwambi ni heri maisha ya kijijini kuliko haya ya mjini yaliyojaa udhia.

Asna anasema kuwa atafuatana na maisha ya mjini pachapacha sawia na mbwa na msasi hadi waliangushe windo. Sara amtahadharisha kwamba, wakati mwingine mwindaji huwa mwindwa. Anamwambia kuwa, maisha ni mshumaa uso mkesha. Asna anashikilia lake na kusema hata wao, wazazi wake, walijitaabisha na kuwasomesha na hawawe kurudi huko huko vijijini na kuishi kama yeyote Yule; lazima wapambane na maisha. Anasema maisha ni kujaribu.


Sara anaona kuwa Asna ana dhiki nyingi kufikia kukonda kama ng’onda lakini Asna anasema huo ni mtindo wa kisasa. Msichana akiwa vile, anapendeza sana. Hili lamfanya Sara kumwambia kwamba, kama anapendeza basi, amletee mtu mtu ili amnunulie leso. Ana maanisha kwamba Asna apate mume aolewe. Asna anamfanyia mzaha na kusema kuwa Bunju tayari amemnunulia Sara leso. Sara asema yake haitoshi. Asna anabisha na kusema kuwa sio kutosha haitoshi bali Bunju ni mkono birika.

Sara anamtetea Bunju kwa kusema ‘mgala muue na haki umpe. Anasisitiza kuwa Bunju amefanya mazuri yake japo Asnas hayaoni. Sara analinganisha hali hii na gari linaloenda kwa gia Fulani na lazima libadilishwe la sivyo litapiga resi tu. Ana maana, ameshavaa leso ya Bunju hadi ikazeeka na sasa ni wakati wa kuivaa ya mumewe Asna.


Neema anajiunga na Asna na Sara na mazungumzo yao yanaendelea huku Sara akiuliza habari za Lemi na Bunju. Neema na Asna wanamshangaa Sara kwa kuwa kila mara huulizia habari za Bunju. Sara anamwambia Asna kuwa akipata mume, Sara atakuwa anaulizia habari zake pia.


Swala la ndoa halimkai vyema Asna. Anaonekana kuogopa kuolewa asije akapewa amri na masharti kama aonavyo Neema akipewa na Bunju. Neema anasema kuwa ng’ombe hashindwi na nunduye na kuwa, hakuna mtu aliyekamilika maishani. Sara anashikilia kuwa Bunju alishafanya mengi mazuri kuanzia na kumnusuru Neema katika ajali ya bararabarani. Yamkinika Bunju alimpata Neema akiwa majeruhi, akamwokoa na kumpeleka hospitalini. Pia alimlipia gharama zote za matibabu.


Asna na Neema hawaelewi ni kwa nini Sara hawezi kulala nyumbani mwa Neema na wako na nyumba kubwa. Asna anona kuwa Bunju amekosa ukarimu ilhali Sara alimpa bintiye(Neema) aliye na elimu ya juu-digrii mbili. Hata hivyo, Neema anashukuru kwa kuwa mumewe amemwachia nafasi ya kutumia mshahara wake atakavyo. Sara anawaambia kuwa, siku zote paka wa nyumba hawingwi. Anaendelea kuwaambia kuwa, Bunju si mume na shemeji tu kwao bali pia ni ndugu yao. Anawakumbusha kuwa Bunju na Neema wamewajengea nyumba kule kijijini. Kuhusu kulala kwake nyumbani mwa Neema, Sara anasema kwamba mila hairuhusu hili.

Mwisho wa onyesho ufikapo, watatu hawa wanakubaliana kufanya hima kuondoka angalau wamwahi daktari ili amtazame Sara. Sara anamalizia kwa kuwaambia wanawe kuwa, mambo ya nyumba kunga, makuti ni kuungaunga. Ana maana kuwa, maswala ya kindani ya nyumba yana kaida zake; hayaanikwi hadharani. Kwamba heshima za familia(nyumba) hudumishwa kwa kuyaweka siri maswala yake. Methali hii ya Kiswahili humaanisha, nyuma(familia) ni siri(kaida) lakini sio jengo lenyewe. Jengo huundwa tu kwa vifaa kama vile makuti n.k ndiposa methali yasema ‘makuti ni kuungaunga’.

Advertisement

Next: Sehemu ya Tatu >>

Related Posts

Facebook

Get the Facebook Likebox Slider Pro for WordPress