Mwongozo Bembea ya Maisha sehemu ya tatu

Previous <<Sehemu ya Kwanza

Previous <<Sehemu ya Pili

Mwongozo Bembea ya Maisha sehemu ya tatu. Waweza kufuatilia sehemu ya kwanza na ya pili kwa kubonyeza hapo juu.

SEHEMU YA III


ONYESHO I


Bembea-ya-maisha
Bembea ya Maisha

Nyumbani kwa Neema. Mwenyewe Neema anaonekana kuzidiwa na mawazo. Anajisemea huku akiyakashifu madhila yaletwayo na maradhi. Anasema kuwa maradhi yana madhila mengi na wakati mwingine huchezhea dawa mwajificho; dawa ikiingilia huku maradhi hutokea kwingine. Analalamikia namna pesa zinavyotumika katika matibabu. Yamkini, amesukumwa sana na maradhi ya Sara hadi kufikia kupungukiwa na pesa.


Bunju anaingia akiwa nadhifu sana. Haichukui muda, wawili hawa wanarejelea mazungumzo yao ya kawaida kuhusu pesa na matumizi yake. Neema anamwomba Bunju amtilie pondo angalau mzigo wa mama uwe mwepesi kwake Neema. Bunju anashikilia kwamba hana pesa kwa kuwa ana mzigo mkubwa wa familia hii yake. Anamwambi Neema kwamba maneno yake sasa yanamchosha na ni kana kwamba haielewi hali ya Bunju.

Neema anaomba hata angaa apewe mkopo na Bunju lakini mwenzake huyu anamwarifu kuwa mambo ya ngomani huishia hapo; kwamba, mjadala kati yao kuhusu pesa na mahitaji ya Neema ulikwishafungwa. Neema anamwabia Bunju kuwa amepungukiwa na pesa za kumtoa mama hospitalini. Bunju anamwambia kuwa angependa sana kunsaidia lakini hakuwa na uwezo huo. Anamwambia Neema ni afadhali yeye kwa kuwa ndio mwanzo ameanza kukopa, yeye Bunju ana madeni chungu nzima. Neema anakubaliana naye na aelekea kuielewa hali ya Bunju.
Ghafla, Bunju anakumbuka kuwa alikuwa na miadi na bwana mmoja na anaamua kuondoka. Anamwambia Neema kuwa, mambo yakienda vizuri(katika miadi hii) atampiga jeki.


Bunju atokapo, Neema anabaki kujisemea tena. Anayakumbuka maneno ya Sara kuwa Bunju ni mmoja wao. Anaelekea kuufahamu ukweli ulioko katika maneno haya. Anasema kuwa mwenye macho haambiwi tazama. Anakuja kuona kuwa, kwa kweli Bunju ni zawadi kubwa kwa familia yao na kuwa amewasaidi pakubwa. Anashangaa kama sio Bunju, familia yao ingekuwa vipi leo. Anakumbuka tena namna Bunju alimwitishia ndege ya ‘flying Doctors’ kumpeleka hospitalini pale alipopata ajali. Zaidi ya yote, alimlipia gharama zote. Kwa hili anashangaa, ni vipi tena Bunju asiwe zawadi kwake.

ONYESHO II

Advertisement

Hospitalini. Neema na Asna wamefika kumjulia hali Sara. Sara anaonekana kuwa nafuu kiasi ila alalamika kuwa dawa zamtia uchofu. Anataka atoke hospitalini kwa kuwa gharama zinapanda lakini wanawe wanamwambia heri wafilisike lakini apate afueni. Tunakuja kufahamu kwamba yupo katika hosiptali ya kibinafsi ambayo tofauti na zile za umma, matibabu ni ya hali ya juu. Sara mwenyewe anakili kuwa huduma pale ni bora kuliko za hotelini hadi mtu anashindwa kuamini kama yumo wodini. Analinganisha na hospitali za kijijini na kusema zile za kijijini ni kana seli. Asna anamuunga mkono na kusema hata wahudumu wa hospitali za kijijini hawana mlahaka mwema na wagonjwa. Kilichoko ni amri na vitisho.


Sara anaulizia hali ya Lemi na kuambiwa kwamba hajambo. Asna anasema kuwa amekuwa mkubwa siku hizi na mwerevu. Sara ansema kuwa ana akili kama zake. Sara anasema kwao wana akili zinazotoia na kutoa kama mashine. Neema anamkumbusha kuwa, Yona naye husema zake ni sumaku haswa.


Sara anaonekana kuwa yuko tayari kwa lolote hata kufa asemapo kuwa anashukuru kumwona Lemi kabla ya kuondoka. Kuondoka hapa kuna maana ya kufa. Wanwae wanamkanya kuwa na mawazo kama hayo na kumhakikishia kuwa atapa nafuu. Anawaambia wanawe kuwa mauti yakija hawatafanya lolote lakini nao wamwambia asiyaalike; yaje tu yenyewe.


Ni dhahiri kwetu kwamba, hii ni siku ya nne ya Sara tangu alazwe. Anahofia biashara zake. Aakumbuka mtama wake ambao hajui kama umevunwa na kama ulivunwa, shughuli hiyo iliendaje. Anamfikira Yona pia na kuona kana kwamba anahangaika. Anamwonea huruma kwa kuzidiwa na kazi nyumbani; kuku, mbuzi na ng’ombe. Anahofia pia kwamba pengine maji yamekwisha na hakuna wa kwenda kumtekea. Asna anabisha kwamba Yona bado ni kijana anaweza kuteka maji. Hili linamshtua sana Sara anayesema kwamba Yona hawezi kwenda kuteka maji. Anauliza wazee wenzake wakimwona watamwonaje? Kijiji kitasema nini?

Sara anahofia watu watasema kuwa yeye(Sara) anewekwa jijini ili baba yao ataabike. Anaona kuwa kwa hili watu watamtazama Yona kwa sini ya dharau.
Sara anasema kuwa yeye anakula vyema pale alipo na pia anahudumiwa ila Yona hana wa kumhudumia. Kwa hivyo, anataka kuondoka na kurejea kijijini.
Mara mazungumzo yanamrejela Bunju. Sara auliza kwa nini hajaja kumwona. Anaarifiwa kuwa Bunju alikuwa na shughli nyingi. Sara anakubali na kusema kuwa Bunju ana bidii ya mchwa lakini Asna anabisha hili na kusema kuwa Bunju hana murua. Sara anamtetea na kusema kuwa hajaona Bunju kakosa adabu.

Asna anabisha zaidi na kusema kuwa Bunju hana adabu na pia ana ubaguzi na moyo mgumu kama jiwe. Anasema Bunju amejaliwa lakini bahili kama mchanga wa dhahabu. Hili linamkasirisha Sara na kumwonya Asna kwamba, huenda akamvunjia Neema nyumba. Asana anabisha kuwa Bunju ana uwezo lakini hataki tu kutoa. Neema naye analalamika kwamba Asna huona kana kwamba hakuchagua mume vizuri. Anasema kuwa, alikwisha kuchagua na tayari ana watoto wa Bunju. Nyuma hakurudiki. Anasema kuwa yeye anamwelewa Bunju kwa kuwa ni kitindamimba. Amelelewa na wakubwa wake. Na wakubwa wake hao wanayashughulikia mahitaji ya wazazi wao. Kwa Bunju, familia ni bibi na wanawe. Neema anasema mara ya kwanza alipatwa na culture shock. Vile vile, Banju alipatwa na mshtuko uo huo kutokana na tofauti zao za mila.

ONYESHO III

 Onyesho hili lianzapo, Neema anamsaidia Lemi(mwanawe) katika masomo yake. Lemi analalamika kwamba kwa muda mrefu wazazi wake hawajampeleka ziara. Neema anamweleza mwanawe kwamba hataweza kumpeleka ziara kwa kuwa anamrudisha bibi kijijini. Lemi anashangaa ni kwa nini bibi yake hakuja kumsalimia.

 Neema anafululiza hadi kwa mumewe na kumwomba ampeleke Lemi kwenda kuogelea kwa kuwa yeye anapanga kumrejesha mama yake nyumbani. Bunju anakataa kwa sababu ya gharama na pia anasema anaenda kutafuta riziki. Analalamika kuwa Neema mara nyingi yuko nje kikazi na anamwachia majukumu yote ya nyumbani.

 Bunju analalamika kwamba hakujulishwa kuwa mama mkwe ametoka hospitalini na kwamba atasafirishwa kijijini. Neema anamwambia Bunju kuwa hakutaka kumsumbua na mambo ya kwao nyumbani.

 Kulingana na Bunju, Neema ameanza kumdharau. Bunju anamkumbusha Neema alivyokuwa mahututi wakati alipompata. Suala hili linamhuzunisha Neema hata anaanza kulia. Bunju anamhurumia na kumwambia atulie asilie mbele yake.

Kwa mujibu wa onyesho hili, tunashuhudia mivutano kati ya wanandoa kuhusu majukumu ya familia yao. Ni bayana kwamba suala hili linahitaji tahadhari ili lisiwe chanzo cha mafarakano katika ndoa. Pia, kuna suala la gharama za kulea watoto. Ni lazima wazazi wawape muda wana wao kama Neema anavyomsaidia Lemi na kazi za shule. Lakini pia kuna gharama nyingine za kuwafurahisha watoto ambazo zinahitaji pesa na mara nyingi pesa hizo hazipo. Kwa hivyo, ni lazima kuwe na maelewano baina ya wazazi na watoto kuhusu mambo hayo ili kusiwe na mikurumbano.

Advertisement

ONYESHO IV

Sara na Asna wanazungumzia juhudi za Dina na wanawe ambazo zimewasaidia kujitoa katika lindi la umaskini.

Onyesho hili la nne linatukia nyumbani kwa Asna. Asna na mamake wana mazungumzo yagusiayo masuala kadha. Kutokana na mazungumzo baina ya wawili hawa, ni wazi kwamba Asna hana imani na asasi ya ndoa. Yaelekea anaridhika na maisha aishiyo ya kuwa bila mume japo amafekia umri unaomruhusu kuolewa. Kulingana naye, ndoa kati ya Neema na Bunju ina kasoro kwa kuwa Bunju ni bahili na hapendi wazazi wa Neema walale nyumbani kwake. Juu ya hayo , anaonaa kuwa, mama yake pia aliteseka sana katika ndoa yake. Ana wazo kuwa ugonjwa alionao Sara ulitokana na kero za Yona, baba yao. Kutokana na madhira ayaonayo katika ndoa hizi mbili, Asna anaamua kuishi nje ya ndoa. Katika onyesho hili, Sara anapata muda wa kumzungumzia Asna masaibu ya ndoa yake na babake na jinsi yalivyoanza. Sara anamweleza kuwa ingawa ndoa huwa na changamoto nyingi, uvumulivu huwasaidia wanandoa kukabiliana na changamoto hizo.

 Kulingana na Sara, bidii ni silaha inayoweza kumkomboa mwanadamu kutoka umaskini. Familia ya Dina inatumika kama mfano wa familia ambayo awali ilikuwa maskini lakini ikafaulu kujinyanyua kutoka hali hiyo ya umaskini na kujikimu ipasavyo.  Sara anamweleza Asna kuwa hata yeye (Sara) na mumewe Yona walikuwa maskini lakini hawakusita kufanya bidii. Waliungana katika juhudi zao ili kujimudu katika kuwatunza na kuwasomesha watoto wao hasa wakati Yona alipopoteza kazi yake ya ualimu. Hatimaye, watoto wao waliweza kuhitimu hadi Chuo kikuu. Inamsikitisha kuwa wanajamii bado waliwachukulia kuwa maskini wa kutojaliwa kupata mtoto wa kiume hata baada ya kufanya juhudi hizo zote.

Sehemu IV

Onyesho I

 Onyesho latukia kijijini nyumbani kwa Luka. Luka anawakaribisha rafikize, Beni na Yona kwa sherehe ya kufurahia mazao yake. Beni alalmikia jinsi watu waliotupa mila zao. Anahofia kwamba vizazi vijavyo havitakuwa na mila na desturi. Katika mazungumzo yao, wazee hao watatu wanakubaliana kuwa vizazi vya siku hizi vinafikiria kuwa uzungu ndio ustaarabu. Jambo hilo linatokana na malezi ya mjini ambayo mara nyingi yameachiwa wafanyakazi wa nyumbani. Wazazi wanaraukia vibaruani asubuhi na kurudi usiku watoto wakiwa wameshalala.

 Luka anawakumbusha wenzake kuwa mila za zamani hazikuwaruhusu watoto wa kike kwenda shuleni wala kurithi mali ila walitegemea usaidizi wa waume zao. Lakini anakubali kuwa thamani ya mtoto wa kike imepanda na nafasi yake kupanuka. Watoto wa kike wa Yona wanamulikwa katika mazungumzo haya. Japo walidharauliwa hapo awali, sasa wamekuwa nyota ya jaha. Ni wazi kwamba wao sasa ndio wanaogharamia matibabu ya mama yao katika hospitali za hali ya juu huko mjini.

 Hata hivyo, fikra za kitamaduni bado zinatawala. Beni anamlaumu Sara kwa kumwacha Yona peke yake akifanya kazi zote za nyumbani. Luka anapinga kauli ya Beni ya kuwadunisha watoto wa kike na mwanamke kwa jumla.  Katika onyesho hili, masuala ya ulevi na athari zake, taasubi ya kiume, usawa wa kijinsia na mabadiliko yanaangaziwa.

Onyesho Il

 Onyesho hili linatokea nyumbani kwa Sara, kijijini. Sara na Neema wanajadiliana kuhusu suala la utamaduni na mabadiliko ya kijamii.

 Neema anasema ulimwengu unakwenda mbio ilhali watu wengine wamebaki nyuma katika mielekeo ya kijadi ya kubugia pombe bila kikomo.

 Sara anamtetea Yona kwa kutowajibika ipasavyo na majukumu ya nyumbani hasa yale ya mifugo. Kulingana na Sara, mwanamume hawezi kuwekwa katika kiwango kimoja na mwanamke. Anasema

 Yona anatekeleza majukumu yake ipasavyo. Hizo ni fikra za kitamaduni. Kwa Sara, mwanamume ana nafasi yake katika jamii na hapaswi kumsaidia mwanamke kazi za nyumbani. Kufanya hivyo ni kualika minong’ono ya wanajamii na kuwakosesha wanawe waume wa kuwaoa.

 Sara anatunza heshima ya ndoa yake ili watoto wake wapate fanaka maishani licha ya mateso anayopata kutoka kwa mumewe. Sara anampa Neema ushauri unaoweza kuifanikisha ndoa yake. Anamshauri Neema azungumze na baba yake kwa hekima ili amsaidie kubadilisha msimamo wake, hasa kuhusiana na ulevi.

Onyesho III

Onyesho linafanyika asubuhi pale kijijini. Yona yuko peke yake sebuleni. Ugonjwa wa mkewe unamhuzunisha na anajutia maisha yake ya awali yaliyomletea mkewe ndwele. Neema anampata babake akiwa katika hali ya mawazo mengi. Yona anashangaa kumwona bintiye amekonda.

na anamwelezea Neema jinsi maradhi ya Sara yalivyoathiri mji wake. Anamshukuru kwa kumshughulikia mamake.Yona anakumbuka maisha yake ya chuoni na jinsi alivyokuwa mwerevu. Neema anapata mshangao anapogundua kuwa babake ameandaa kiamshakinywa mapema, yeye na mama yake wakiwa bado wamelala. Neema anafurahi na kumshukuru babake kwa wema wake.

Onyesho linaisha kwa kuonyeshwa Yona akiomba msamaha kwa Neema kwa makosa aliyowafanyia wakiwa wangali wachanga. Yona anatumai kuwa mabinti wake wengine watamsamehe siku moja. Yona pia anaomba msamaha kwa mke wake na kumwahidi kuwa asitie shaka atakuwa naye katika kila hali. Taa zinazima na wote watatu wanakumbatiana kuonyesha hali ya kusameheana na kuja pamoja kwa familia hiyo.

Next: Maudhui >>

Advertisement

Tazama Maudhui

Related Posts

Facebook

Get the Facebook Likebox Slider Pro for WordPress