Bembea-ya-maisha

Huu ni Mwongozo wa Bembea ya Maisha, tamthilia iliyoandikwa na Timothy M. Arege, mwandishi aliye na tajriba kubwa ya uandishi. Arege ameandika vitabu vingi ikiwemo tamthilia mashuhuri ya Mstahiki Meya iliyokuwa tamthilia teule kabla ya ujio wa Kigogo.

Katika sehemu ya kwanza, tutaangazia muhtasari wa maonyesho. Sehemu ya pili itaangazia maudhui.


Katika huu Mwongozo wa Bembea ya Maisha tutaangazia maswala yajitokezayo katika kazi yake Timothy Arege. Tamthilia hii inahusu mwanaume kwa jina Yona na mkewe aitwaye Sara. Wawili hawa wameyapitia magumu mengi ya maisha na kuweza kuyavumilia na kuvumiliana wenyewe. Maisha yao yamekuwa na pandashuka nyingi jambo lililo kawaida maishani.
Wawili hawa waliooana na kuishi vizuri ila hawakujaliwa watoto kwa wakati uliotarajiwa . Hili liliwafanya watu kuwasema sana. Waliwaona kama waliokuwa na udhaifu fulani. Baadaye walijaliwa watoto . Wajuaji wakabaki vinywa wazi. Hata hivyo, kwa vile hawakujaliwa watoto wa kiume , watu walianza kuwasema tena.

Kwa kuwa kulingana na desturi ya kiafrika, mtu hurithiwa na mtoto wa kiume, watu waliulizana Yona atarithiwa na nani. Kutokana na hofu nyingi; hofu ya kutotaka kusemwa, hofu ya kushindwa na kuonekana dhalili, Yona alishinikizwa kuoa mke mwingine japo alighairi. Badala yake, alimwelekezea mkewe hasira na akawa anamchapa, wakati mwingine vibaya sana. Zaidi ya yote, Yona aliupokea ulevi kwa mikono miwili – kama asemavyo Dina. Yona alizidi kusukumwa na watu atafute mtoto wa kiume hata kama ni nje ya ndo, bora tu awe wa kiume. Kinyume na maoni ya wengi, wanawe wa kike wa Yona waliibuka kuwa hodari masomoni na wakafaulu vizuri na kuweza kuwatunza wazazi wao uzeeni.


Hadithi hii pia inamwangazia pia Banju na mkewe Neema. Neema ni kifungua mimba wa Yona na Sara. Ameolewa na Banju ambaye ametoka katika jamii iliyo na desturi tofauti na ile ya kina Neema. Kwa mujibu wa desturi ya kina Banju, mama mkwe hawezi kulala kwa bintiye aliyeolewa. Tofauti hizi za kidesturi kati ya Banju na Neema zinaleta mzozo kati ya wawili hawa. Kila mmoja anaona ugeni na ajabu kwa desturi ya mwenzake. Banju anamruhusu Neema kutumia mshahara wake apendavyo-kuwakimu wazazi wake na haswa kumtafutia matibabu mamake anayeugua(Sara). Zaidi ya hapo, haoni haja ya kubebeshwa mzigo wa familia ya Neema(mkewe). Hili linamfanya Neema kutomwelewa kwa kuwa alimtaraji ampige jeki katika matibabu ya Sara. Banju naye anasema ana majukumu mengi na hawezi kumudu mahitaji yote ya kifedha haswa yanayohusu familia ya Neema. Asna, dadake Neema anaonea jambo hili ajabu na kumwona Banju kama mtu hasidi. Jambo hili pamoja na kipogo alichoona babake akimpiga mamake, kinmtia hofu ya kuolewa. Tangu hapo, Asna anona ndoa kuwa kama kifungo au utumwa wa aina yake na anaapa kutoolewa. Hata hivyo, mama yake anamwambia kuwa, yaliyotokea kwa ndoa ya mtu mmoja si lazime yatokee kwa ya mwingine. Anamwambi Asna (Uk54) Kuwa ndoa ni bembea. Kuna wakati itakuwa juu na wakati itakuwa chini. Anamsihi Asna atafute mume aolewe na kumpa Sara wajukuu.

Advertisement

Kilele cha hadithi hii ni kuwa, Sara anamtetea Yona licha ya kumchapa na kumsababishia maradhi ya moyo. Anasema (Uk 66) mgala muue na haki yake umpe. Anasisitiza kuwa, Yona wakati mwingine hutenda mambo mazuri nay a kumsaidia Sara. Huingia jikoni anapojisikia, huweka tarehe ya mikutano ya vikundi vyao na huhudhuria vikao vyote. Msimamo huu wa mama unambadilisha Neema na mtazamo wake kwa baba yake na anaamua kubadilika. Sara anasihi Neema kutumia usasa alionao pamoja na utamaduni kubadilisha mambo. Anamwambia aaanze na babake na badala ya kumkabili, ajaribu kumshawishi. Wakati uo huo, Yona anajirudi na kuyaona makosa yake. Anamwonea huruma mkewe kwa taabu anazopitia kutokana na maradhi yake. Yona anajutia maisha ya jana yake na namna alivyoyaishi. Anasema laity angalijua, angaliishi tofauti. Anafikia uamuzi wa kuyabadili maisha yake na kuachana na ulevi. Anaipa pombe buriani ya milele. Neema ajapo kumshawishi, anapata Yona amebadilika tayari na hata amweaandalia kiamshakinywa. Wote watatu, Yona, Sara na Neema wanakumbatiana.

Bembea Ya Maisha
Bembea Ya Maisha

MUHTASARI WA MAONYESHO


SEHEMU YA KWANZA


ONYESHO I

Onyesho hili linatokea wakati wa alasiri nyumbani kwa Yona na Sara. Onyesho lianzapo, tunamwona Sara akimeza vidonge vya dawa ana hapo ndipo Yona anaingia na kujiunga naye. Yona ametoka kwa wazee wenzake na anarejea nyumbani akitaraji kuwa mkewe ameandaa chakula. Hata hivyo, Sara namna alivyo, hawezi kuandaa chochote kutoka na maradhi yake. Badala yake, anamtarajia Dina rafikiye, aje amsaidie kuandaa chakula. Yona na Sara wanaingia katika mazungumzo yanayowahusu watoto wao.


Inadhihirika kwamba, wana mtoto aitwaye Neema ambaye amekuwa akiwasaidia kwa fedha. Hulipia matibabu ya mama(Sara) na kumpa Yona pesa za matumizi asiaibike mbele ya wazee wenzake. Yamkinika pia kwamba, Yona anaona kuwa Neema apaswa kujitwika wajibu wa kuwalea wazazi wake; anakuita kuirithi fimbo yam zee kwa kuwa ndiye motto wa kwanza. Kinyume chake, Sara ameshikilia desturi yao kwamba anayepaswa kurithi fimbo yam zee ni mtoto wa kiume.

Kwa upande wake, Yona haoni kubwa ambalo Neema amefanya japo amewalipia wanuna wake karo na kuwaajiria wafanyakazi wawili. Amwambiapo Sara amwite Neema kumpeleka hospitalini, Sara asema motto aachwe apumzike. Yona hakubaliani naye na anauliza kana kwamba yeye(Yona) alimpuzika alipokuwa akimpeleka shuleni. Mfanyakazi wa kwanza aliondioka akidai palikuwa na kazi nyingi ilhali wa pili walimsimamisha kazi kwa kukosa uaminifu. Katika mazungumzo yao, Yona anashuku kwamba Sara amekuwa akimchonganisha na wanawe jambo ambalo Sara amelikanusha na kusema kwamba si hulka yake hiyo. Tena, haoni haja ya kuuvunja mji. Sara analalamika kwamba, kila mara wakizungumza, lazima Yona arudi pale pa ‘watoto wako’. Anamuuliza Yona kana kwamba wale watoto si matunda ya ushirikiano wao. Jambo hili linaakisi hali ambapo wanaume katika jamii huwachukulia watoto kuwa wa akina mama. Mwishoni wanakubaliana kumpa Neema Baraka zao.

Advertisement

ONYESHO II


Onyesho la Pili linatokea nyumbani kwa Dina ambapo Kiwa mwanawe amefika kumjulia hali mamake. Kutokana na mazungumzo ya mtu na mwanawe, tunafahamu kwamba, Kiwa hapendi kula sana na amekonda sana. Anajitetea kwa kusema kwamba ardhi ya kulima imeadimika sana nayo mvua haipatikani. Kiwa anaendelea na kusema kwamba ulimwengu wa sasa hautambui kimo, badala yake akili huwa muhimu zaidi. Anataja Neema binti Yona kama mfano mwafaka-anamlinganisha na chuma ya reli kwa wembamba wake. Dina naye amsifu Neema kuwa zaidi ya kuwa kama sindano kwa kimo, ana akili ya ncha ya sindano.
Dina anamsimulia Kiwa kuhusu maisha ya zamani ya Yona na Sara. Anamweleza kuwa, wawili hawa walichumbiana kwa mapenzi tele na hatimaye kuoana. Hata hivyo, walipochelewa kupata watoto, watu waliwatia vinywani na kuwasema sana. Mwishowe walipojaliwa watoto waliowasema walibaki vinywa wazi lakini hali ilibadilika punde baadaye.

Watu walianza kuwasema tena kwa kuwa hawakupata wana wa kiume. Waliulizana, Yona atarithiwa na nani? Wakwa wanawasema tena. Mara hii, Yona alishinikizwa kuoa mke mwingine ili abahatishe kama tapata mwana wa kiume. Wengine walimshinikiza kupata mtoto nje ya ndoa aone kama atapata wa kiume. Kutokana na hofu ya kusemwa, kushindwa na kuonekana dhalili, Yona aligeukia pombe na kuifanya mwenziwe. Vile vile, alimwelekezea Sara kipigo kwa kukosa kumzalia mwana wa kiume; wakati mwingine alimpiga vibaya sana hadi kufikia kumwagiwa maji baridi kumrejeshea fahamu. Mwishoni mwa Onyesho, Dina anaondoka kwenda kuitikia wito wa Sara wa kumsaidia kuandaa chamcha.

ONYESHO III


Onyesho la tatu linatokea nyumbani kwa Sara. Dina amefika kumsaidia Sara katika upishi. Kutokana na mazungumzo yao, tunaelewa kwamba, maradhi ya Sara yamesababishwa na mawazo pamoja na mateso apatayo kutoka kwa mumewe. Hata hivyo, Dina anamwambia ashukuru kwa kuwa ameugua wakati ako na motto anayeweza kumuauni; vinginevyo mambo yangekuwa mabaya zaidi. Kwa mujibu wa wawili hawa, mtoto wa mtu ni kama mwokozi wake; hii ina maana kwamba, Neema anamwokoa Sara kutokana na masaibu ya maradhi. Sara vile vile anayaona maisha ya motto wa kiume kama yanayotawaliwa na ubabe ndume. Kutokana na vile motto wa kiume analelewa, kuna mambo ambayo hawezi kuyafanya kwa kuwa amefundishwa kuwa huo sio wajibu wake. Kwa mfano, Yona hawezi kumsaidia Sara kazi za nyumbani japo anaugua kwa kuwa akifanya hivyo atasemwa na watu.

Mazungumzo yao yanapoendelea tunafahamu kwamba, kulikuwa na mpango wa Neema kuja keshoye kumchukua mamake ili ampeleke hospitali. Ni wazi kwamba atakuja kwa gari lake mwenyewe jambo ambalo linamshangaza sana Dina anayeshangaa kama kweli Neema huliendesha mwenyewe hata huko mjini.

Bonyeza hapa uelekezwe katika sehemu ya pili.

Next: Sehemu ya pili >>

Facebook

Get the Facebook Likebox Slider Pro for WordPress