info@kwiksaf.com

+254797418099

May 29 24

Nguu za Jadi – Mwongozo

Kibe
Nguu-za-Jadi-jalada

Utangulizi wa Nguu za Jadi

Nguu za Jadi ni riwaya teule kwa shule za upili nchini Kenya na ya mwisho katika mfumo wa elimu wa 8-4-4. Riwaya hii imeandikwa na Clara Momanyi, mwandishi aliye na tajriba kubwa katika fasihi ya Kiswahili.
Katika Makala haya ya mwongozo wa Nguu za Jadi, tutaangazia maswala yote yanayohusus riwaya hii teule kwa lengo la kumwelekeza mtahiniwa wa K.C.S.E kuweza kuyamudu maswali ya mtihani.
Mwongozo huu ni wa kuelekeza tu, bali sio kibadala cha kuisoma riwaya. Sharti mtahiniwa aisome riwaya hii, na ikiwezekana, aisome mara kadha ili kuweza kujiandaa vyema kwa mtihani wake.

Maswala Makuu

Makala haya ya mwongozo wa Nguu za Jadi yataangazia maswala yafuatayo:

  1. Jalada la riwaya.
  2. Ufaafu wa anwani ‘Nguu za Jadi’.
  3. Muhtasari wa sura kwa sura.
  4. Dhamira
  5. Maudhui
  6. Wahusika
  7. Mbinu za lugha na Sanaa.
Nguu za Jadi

Jalada la riwaya ya Nguu za Jadi ina picha kadha ambazo zaweza kufasiriwa kwa njia mbalimbali. Baadhi ya picha/michoro hii ni:


a) Giza. Jalada la riwaya hii lina mwangaza hafifu. Michoro yote katika jalada imegubikwa na kiwango fulani cha giza au ukungu wa aina yake. Hii yaweza kufasiriwa kama dalili ya vile jamii husika imegubikwa na giza la ujadi. Giza la ukabila, chuki, dhuluma miongoni mwa maovu mengine.
b) Mwanaume mzee na kijana. Picha moja katika jalada ni ya mwanaume mzee aliyekiti kwa kiti na kijana aliyeka chini ardhini. Yamkinika mzee huyu anashauriana na kijana aliye mbele yake ambaye aonekana kuwa makini kwa ayasemayo mwanaume huyu. Hii inaweza kuchukuliwa kama ishara ya mtoto wa kiume ambaye ametanzwa na matatizo, ambaye hajapewa hadhi anayostahili katika jamii, kama inavyoonekana baadaye kwenye riwaya yenyewe.
c) Mimea. Picha nyingine ipatikanayo katika jalada hili yaonyesha uwanja usiokuwa na mimea, ishara ya uharibifu wa mazingira katika eneo la Matango.
d) Mlima na Vilele. Pichani pia mna mlima mkubwa ulio na vilele(nguu). Ishara ya vikwazo vinavyoitatiza jamii ya Matango.
e) Mwangaza. Nyuma ya mlima mna mwangaza hafifu. Mwanga huu unaweza kuchukuliwa kuwa kiwakilishi cha matumaini mapya. Ni ishara kwamba jamii iliyokumbwa na matatizo mengi kwa muda mrefu hatimaye inapata mwanga, kama inavyofanyika kwenye riwaya Lonare anapochaguliwa kuwa mtemi, jambo linaloipa nchi ya Matuo matumaini mapya ya mabadiliko chanya.

Ufaafu wa Anwani ‘Nguu za Jadi’

Tunapoangazia swala la ufaafu katika muktadha wa fasihi, huwa tunakadiria ni kwa kiwango gani anwani ya kazi ya fasihi ianaakisi yale yanayotendeka hadithini. Anwani ya kitabu, kama Nguu za Jadi, yafaa kuangazia ukweli Fulani au maswala makuu yanayozingatiwa katika kazi husika.
Kulingana na kamusi, nguu ni kilele au sehemu ya juu kabisa yam lima. Katika riwaya yetu hii, neno nguu limetumika kuwakilisha vikwazo vinavyoikumba jamii ya Matuo. Nguu za Jadi basi ni vikwazo ambavyo vimekuweko tangu zamani. Vikwazo hivi ni kama vile desturi au kanuni za maisha, mahusiano katika ya makundi ya jamii, mambo ambayo yanatatiza maendelea na ufanisi wa jamii.

Nguu husika hapa ni zipi?

Baadhi ya matatizo na vikwazo katika riwaya hii ni kama vile:

  • Uongozi mbaya unaodhihirishwa na Mtemi Lesulia na vibaraka wake kama Chifu Mshabaha.
  • Mila zinazolemaza na kudunisha wanawake kwa kuwanyima uhuru ya kujiamulia mambo.
  • Ukabila na chuki za kijamii zinazojitokeza kati ya Wakule na Waketwa.
  • Ubaguzi wa, ufisadi, utabaka, ubadhirifu, ukiukaji wa haki za watoto miongoni mwa maovu mengine.
  • Ulanguzi wa dawa za kulevya na ulevi.
  • Changamoto za ndoa.

Hivi ni baadhi tu ya vikwazo vinavyojitokeza riwayani na ambavyo vinatosha kuonyeshha kwamba anwani Nguu za Jadi inafaa kabisa kuwa anwani ya riwaya hii.

Muhtasari wa Sura Zote>>

Nguu za Jadi – Sura ya Kwanza

Get In Touch

Kilimani, Nairobi, Kenya

info@kwiksaf.com

+2547974180990

Follow Us

© Kwik Saf. All Rights Reserved. Designed by Kwik Saf Express