ChuoKenya

Mwongozo Wa Damu Nyeusi Part 1

MKE WANGU

Hadithi hii inaanza wakati ambapo msemaji alikuwa anachaguliwa mke atakayeoa na wazee wake lakini hakutaka hivyo yeye alimtaka motto mbichi ambaye angemvumbika mpaka aive. Pia alimtaka mke ambaye alikuwa na sifa ambazo angetaka mke wake awe nazo. Alimweka Aziza rohoni mwake kwani alikuwa kinyume na wasichana ambao walikuwa wamesoma. Alikwa amesoma skuli akapata kuwa mjuaji sana. Msemaji anasema kuwa alipomaliza masomo yake ya juu,mamake alianza kumshawishi kuhusu mambo ya ndoa. Mama alimtajia wasichana kadhaa lakini aliwakataa wote na kusema kwamba alimtaka Aziza aliamua kumwoa.
Baada ya harusi na sherehe walienda fungate yao ambapo msimulizi alipata kumsoma Aziza na apate kumsomesha. Katika harakati ya kumsoma Aziza,msimulizi aliona kwamba Aziza hakuwa na mazungumzo pamoja naye ,pia aliona jinsi alivyokuwa akimtazama kwa unyarafu. Alipoulizwa kwa nini alifanya hivyo,alisema kuwa alimsikitikia kwani alimwona kama gumegume tu wala si mume wake kwa sababu hakuwa anafanya kazi yoyote isipokuwa kutembea tembe.
Aziza aliteta pia kwamba mumewe alikuwa na mikono laini kiasi cha kuwa angemguza mwanamke hangehisi chochote. Aziza hakuwa anavalia viatu kila alipokwenda, na alipoulizwa mbona havalii alisema kwamba hataki kutegemea ngozi za ng’ombe aliyekufa .
Msimulizi anasema kwamba humwamrisha mkewe atakavyo kutamshinda. Pia anasema kuwa anaona fedheha kuu,kwanialio kisonoko ambaye hangeweza kutoka naye mbele za watu alishangaa jinsi atakavyoishi naye mbele za watu. Alishangaa jinsi atakavyoishi naye kwa sababu hata mambo madogo ambayo ni muhimu hatilii maanani.
Aziza alikuwa amenunuliwa brushi ya meno na dawa ya meno lakini hakuvitumia hata kidogo.Aliamua kumuuliza asili yake.
Msimuluzi alipomuuliza kwa nini hakutumia brushi Aziza alisema kwamba ana mswaki wake binafsi ambao ulikuwa umetengenezwa na mnazi na ndani mlikuwemo unga uliokaa kati kati baina ya jivu na masizi. Aziza alisema kuwa hatautia mswaki ule mdomoni ati kwa sababu na manyoya ya nguruwe. Pia alisema kuwa wanaotumia brashi baada ya miezi matatu ama mitano huenda kumwona daktari wa meno.
Siku hiyo, Seluwa mtoto wa shangazi yake aliwatembelea. Wazee wa msimulizi walitaka amwoe Seluwa lakini alimkataa kwa sababu zake. Seluwa na Aziza walikuwa wakitaniana ‘mke mwenzangu’ na pengine ‘wifi yangu’. Wakiwa katika mazungumzo yao Aziza alismskia Bazazi wa madafu akipita huko nje. Msimulizi alimpa Aziza shilingi mbili akanunue hayo,kasha Aziza akamwita Bazazi huyo aende nyumbani mwao.
Bazazi huyo alipofika humo, Aziza akamwambia bwanake kwamba nia ya kumwita huko nyumbani ilikuwa ili aone kuwa alitaka bwana kama huyo. Hayo ni kwa sababu daima alikuwa anafikiri kazi tu. Baada ya kumwambia hayo,Aziza alimwambia bwanake aampe talaka yake.

2. Wahusika
Hadithi hii ya Mke Wangu ina wahusika wafwatao;
Msimulizi
Aziza
Fedhele Salim
Salma
Seluwa
Wazazi wa msimuliza
Wahudumu wa msimulizi k.v Mapanya
MSIMULIZI
Msimulizi ni mhusika mkuu katika hadithi. Alizaliwa katika familia ya kitajiri kama anavyotueleza katika ukurasa wa 18.. Ni kijana wa kisasa na mumewe Aziza.
Ni mtamaduni kwa sababu anautii utamaduni wa jadi unaompendelea mwanamume.
Yeye ni msomi aliyesoma hadi viwango vya juu vya elimu.
Aidha, msimulizi anaweza kuelezwa kama mzembe kwa sababu hataki kujihusisha na kazi za sulubu kama vile kuangusha nazi, kuchoma na kuuza mihogo pamoja na kazi nyinginezo. Anashangazwa na uamuzi wa mkewe wa kutotaka kufuliwa nguo wala kuooshewa vyombo.
Ingawa tumemtaja kama mtamaduni, Msimulizi anaweza kueleweka kama mwanausasa kwa sababu anampendekezea mkewe kutenda mambo ya kileo kama vile kuvaa viatu na kupiga mswaki. Kwa sababu hii, anadhihirisha tabia ya mtu asiye na msimamo dhabiti. Ukosefu huu wa msimamo unamfanya ashindwe kujiamulia mambo muhimu maishani kama vile; mke wa kuoa, kazi ya kufanya na namna ya kuiongoza familia yake changa. Kwa maneno mengine, msimulizi ni mhusika aliyekengeuka na asiyejifahamu.
Isitoshe, msimulizi ni mvumilivu na mwenye subira kwa vile si mwepesi wa kutibukwa na hisia tunadhihirishiwa kuwa anamvumilia Aziza kama mkewe licha ya fedheha anayoipata mbele ya wageni wao wenye ustaarabu wa kimjini. Licha ya Aziza kumdharau, kumwita gumegume na kumsuta kwa kutofanya kazi maishani, msimulizi haonyeshi kuudhishwa na mkewe.
Badala yake, msimulizi anamkubali na kumvumilia mkewe akitaraji kuwa siku moja atazinduka na kuukumbatia usasa na ustaarabu. Aziza anafikia kiasi cha kumwita bazazi wa madafu kasrini mwao, kumsifu bazazi wa madafu mbele ya mumewe na hata kumuomba mumewe talaka. Msimulizi haonyeshi kukasirishwa na maudhi haya yote.
Ni mwenye taasubi ya kiume; hulka hii inadhihirishwa pale ambapo anatarajia kumpata mke ambaye hakwenda skuli. Nia yake ni kumpata mke ambaye hatakuwa katika ngazi moja ya kielimu naye. Tunaweza kuhitimisha kuwa msimulizi hataki mwanamke mwenye ung’amuzi wa usawa wa kijinsia na haki za wanawake. Kwa mujibu wake, matatizo ya ndoa hutokana na midomo na ujuaji wa wanawake.
Aidha, anapanga kumvinya mkewe na kumfunza mambo ya kisasa ya uanagenzi. Anammithilisha mkewe na tunda linalohitaji kuvinywa. Anaonyesha dharau kwa wanawake kwa sababu anawalinganisha na watoto wadogo ambao hawaachi kisebusebu (uk. 21)
Umuhimu wa msimulizi
Msimulizi ni mhusika mkuu katika hadithi hii. Anaakilisha kizazi kilichochanganyikiwa. Kizazi kilichojipata katika nja panda, yaani katikati ya ukale na usasa.
Mbali na kuchanganyikiwa, msimulizi anaakilisha matatizo mbalimbali yanayoikumba jamii ya kisasa kama vile mfumo mbaya wa elimu inayolenga ajira, ukosefu wa ajira, ujuma na uzembe, matatizo ya ndoa na kadhalika.
Msimulizi ni kielelezo cha jamii ambayo inashindwa kuyaelewa mazingira yake. Anashindwa kuuelewa utamaduni wake, mahitaji yake majukumu yake, na hata hamwelewi mkewe.
Waama, ni kupitia kwa mahusiano ya Msimulizi na mkewe ndipo tunabaini kuwa elimu na hekima ni mambo mawili tofauti.

AZIZA
Ni mhusika mwingine ambaye anaweza kuutajwa kama mhusika mkuu. Ni mkewe msimulizi. Tofauti na msimulizi, Aziza alizaliwa na kukuzwa shamba.
Aziza ana sifa zifwatazo;
Kwanza, Aziza ni mdadisi wa mambo. Anamchuja msimulizi na kuugundua udhaifu wake. Ni kutokana na udadisi huu ndipo anagundua kuwa yeye na msimulizi wako na mawazo yaliyobaidika.
Anaumaizi ulelemama wa mumewe wa kutofanya kazi na tabia ya kutegemea wazazi wake. Anadadisi na kugudua viungo vya dawa ya meno; tumbawe, sabuni na arki za peremende kali. Pia, anagundua kuwa mswaki si lolote si chochote bali nywele za nguruwe.
Aziza anaweza kuelezwa kama mhafidhina, anayapinga madai ya msimulizi kwamba riziki ya kazi imekosekana. Yeye anashikilia kuwa mtu hawezi akakosa kazi ulimwenguni, kazi anazozitaj ni kazi za jadi kama vile kuangusha nazi, kuchoma na kuuza mhogo na hata kuchunga punda. Uhafidhina wa Aziza unazidi kujiidhihirisha pale anapokataa katakata kuvaa viatu huku akishikilia kukanyaga chini kote aendako. Anawadharau wanaume wa kimjini enye usasa na mwishowe anajiafadhalisha kuolewa na mwanamume wa shamba.
Mwenye dharau; kila mara, Aziza anamchuja mumewe kwa dharau. Anavidharau viatu, mikono ya mumewe, mswaki na dawa ya meno ya kisasa. Kitendo cha kumsifia bazazi wa madafu mbele ya msimulizi pia ni ishara ya dharau.
Sifa nyingine ya aziza ni kuwa yeye ni mwenye hekima, majibizano yake na mumewe yanadhihirisha hekima tele. Anashangaa ni kwa nini walishwe na wazazi wa msimulizi. Anaumaizi udhaifu uio kwenye dawa ya kisasa ya meno, anashangaa ni kwa nini wale waliotumia dawa ya meno waliyang’oa meno yao kila wakati. Hekima hii inamfanya msimulizi kukiri kuwa mkewe ni mtu asiyeweza kupatwa kiotoni.
Mwenye msimamo thabiti; Aziza anadhihirisha kuwa na msimamo thabiti kwa mambo anayoyaamini. Anakataa kushawishiwa kuukumbatia usasa. Anashikilia na kuyaishi maisha ya jadi hata kama kila mtu aliye karibu naye ameukubali usasa.
Anapojibizana na mumewe, Aziza anajitokeza kama mhusika jasiri. Anakataa kuwekwa chini na mumewe. Hali ya kutopata masomo ya kisasa haimnyimi uasiri wa kuaimama kidete na kuyatoa mawazo yake. Kutokana na ujasiri wake, anamkabili mumewe na kuzishutumu tabia zake bila hofu wala woga. Hatimaye, anamjulisha msimulizi kimasomaso kuwa angetaka apewe talaka yake.
Umuhimu wa Aziza
Aziza amechorwa kama mhusika bapa sugu. Anao msimamo sugu kuhusu utamaduni wa jadi na hakubali kuubadili msimamo huu.
Anawakilisha watu wanaoshikilia msimamo thabiti wa kuutetea ujadi. Aziza anaweza kutazamwa kama mdomo wa mwandishi kwa sababu mwandishi amempa hekima nzito na amewezeshwa kumpiku msimulizi katika migogoro yao mbalimbali.
Aidha, aziza ametumiwa na mwandishi kuutetea utamaduni wa waafrika dhidi ya athari za kigeni kama vile elimu na mavazi.
Aziza ametumiwa kupitisha ujumbe kuwa furaha na utu wa mtu si elimu wala utajiri wala ajira, bali maadili mema, bidii, heshima na mapenzi ya dhati.
Kupitia kwa Aziza, tunajuzwa kuwa mwanamke wa kiafrika amejikomboa kimawazo na anaweza kujifanyia maamuzi tofauti na adhaniwavyo na wanaume wenye taasubi za kiume kama msimulizi.
Maswali
1. Jadili uhusika (hulka na umuhimu) wa msimulizi na wa Aziza
2. ‘Msimulizi na mkewe hawapatani kwa lolote’, jadili kauli hii ukirejelea hadithi fupi ya Mke Wangu.
FEDHELE SALIM, SALMA NA SELUWA wanaweza kuelezwa kama wasichana wa kisasa; msimulizi anawataja kama wasichana waliojaa utamaduni wa kisasa.
Fedhele anaelezwa na msimulizi kama msichana msomi. Ingawa hivyo, tabia yake ya kuvalia kanzu fupi na kuandamana na wanaume hazimpendezi msimulizi.
Salma anadhihirika kama msichana mwenye kujipodoa na marangi ya mashavu na midomo.
Msimulizi anatueleza kuwa Seluwa ana ‘kidomo’ yaani, ni mtu wa kuongea maneno mengi. Isitoshe, katika uk. wa 24, anamtaja Seluwa kama msichana mwenye kujipodoa na kupendeza.anamtaja kama mwingi wa bashasha, mizaha na furaha.
Umuhimu wa Fedhele, Salma na Seluwa
Hawa watatu ni wahusika wasaidizi.
Wanatusaidia kumwelewa msimulizi kwa sababu wanatusaidia kujua ni mambo gani yasiyompendeza msimulizi.
Aidha, sifa zao zinakinzana na za Aziza hivyo basi wanatusaidia kujua hulka za Aziza.
WAZAZI WA MSIMULIZI ni wakwasi kwa sababu msimulizi anatueleza kuwa yeye alizaliwa katika familia ya kitajiri.
Wao ni wahifadhina kwa sababu wanamlea mtoto wao kwa kuongozwa na tamaduni za jadi za kiafrika na hata wanamchagulia mke kwa mujibu wa kaida za jadi za kiafrika. Msimulizi anatueleza kuwa, …wazee wangu, juu ya utajiri wao, hawakupenda kubadili mila zetu… (uk. 18)
Mamake msimulizi anadhihirisha hekima anapomwongoza msimulizikumchagua na kumwoa Aziza. Anapendekeza wasichana ambao anajua msimulizi hatakubali kuwaoa.
Umuhimu wa wazazi wa msimulizi
Wazazi wa msimulizi ni wawakilishi wa utamaduni wa jadi.
Maswali
1. Jadili uhusika wa msimulizi na Aziza
2. Je, Seluwa, Salma na Fedhele Salim wana umuhimu gani katika hadithi
3. Unadhani ni kwa nini mwandishi akatumia anwani ya mke wangu
4. Ni vipengele vipi vya utamaduni wa jadi anavyovipendelea mwandishi.

3. DHAMIRA
Yaelekea kuwa mwandishi ana nia ya kutubainishia kuwa Elimu ya jadi ni bora kuliko mafunzo ya kisasa ya shuleni na vyuoni; hili linabainika tunapoona Aziza akipewa sifa ya kuwa mpevu wa hekima nzuri na mwandishi.
Msimamo wa mwandishi ni kuwa watu wa shamba waolewe na wenzao wa shamba na wale wa mjini waolewe na wale wa mjini. Msimamo huu umetokana na yale anayoyaona katika jamii; migogoro katika ndoa, ubaidi wa kifikra utabaka na mitazamo ya maisha inayokinzana.
Yamkini wimbi la kisasa ambalo limeiacha jamii ya kisasa katika njia panda limemchochea mwandishi kuiandika hadithi hii ili awakumbushe watu kurejelea kaida zao za jadi.
4. MAUDHUI
Mafunzo yafwatayo yanajitokeza katika hadithi ya Mke Wangu.
· Utamaduni
· Usasa na mabadiliko ya kijamii
· Elimu
· Utabaka, utengano na mitafaruku
· Ndoa
· Taasubi ya kiume na matatizo yanayowakumba wanawake
· Ukengeushi

1. Utamaduni
Mohammed Said Abdulla anadhihirisha utamaduni wa aina mbili.
Kuna utamaduni asilia wa Afrika unaoendelezwa na Aziza na bazazi wa madafu. Aziza anaelezwa kama mwenyeji wa shamba. Aidha anatetea na kudumisha mila za kiafrika kama vile bidii kazini. Anashikilia kuyaishi maisha ya shamba kama vile kutovaa viatu.
Anapuuzilia mbali matumizi ya dawa mswaki na dawa ya meno. Anakataa kuathiriwa na utamaduni wa kisasa.
Utamaduni wa kisasa unaendelezwa nawahusika kama msimulizi, Seluwa, Fedhele na Salma.
Fedhele, Salma na Seluwa wanajipodoa kwa vipodozi na rangi za kisasa.
Msimulizi anatetea uvaaji wa viatu, matumizi ya mswaki wa kisasa na dawa ya kisasa ya meno.
Aidha, msimulizi ni mwanausasa aliyeipata elimu ya kisasa, anaishi kwenye nyumba ya kisasa, anatumia mavazi ya kisasa na vipodozi vya kisasa kama vile kitana.
Selume na msimulizi wanaamkuana kwa kuingiana maungoni; mtindo ambao ni wa kisasa.
2. Elimu
Elimu ni mfumo wa mafunzo yanayopatikana shuleni, vyuoni au maishani.
Maudhui ya elimu yameendelezwa kuwili kwenye hadithi ya Mke Wangu.
Kwanza ni yale mafunzo yapatikanayo katika maisha.
Aidha, ipo elimu nyingine inayopatikana vyuoni.
Japo Aziza ni msichana wa shamba, anadhihirisha ukomavu wa hekima. Hii ni ishara tosha kuwa amebobea katikaa mafunzo ya maisha kuhusu maswala ya kazi, ndoa, mahitaji ya jamii na matarajio ya jamii kuhusu wajibu wa mume na mke ndoani.
Msimulizi na Fedhele ni wahusika waliopokea mafunzo ya vyuoni. Wanatajwa kama wahusika waliopokea elimu ya hadi viwango vya juu.
Hata hivyo, elimu hii iliyopokewa na msimulizi inadhihirika kuwa duni kwa sababu haijamwezesha msimulizi kujitegemea. Ni elimu yenye lengo la kupata kazi na wala hailengi kumsaidia mtu kujimudu katika mazingira yake.
Aidha elimu hii inashindwa kumuhami msimulizi na mbinu mwafaka za kuyakabili matatizo ya ndoa. Anashindwa kuidhibiti ndoa yake na Aziza.
Kwa hivyo basi tunaweza kudadavua kuwa mwandishi anaipendelea elimu ya jadi inayompa mtu mafunzo ya maisha dhidi ya ile elimu ya kisasa inayopatikana shuleni na vyuoni.

3. Utabaka na Utengano
Utabaka ni mfumo wa kijamii unaowagawa watu kwenye makundi kutegemea uwezo wao wa kiuchumi au kijamii.
Kwa upande wake, utengano ni hali ya watu kuwa mbali na wengine. Umbali hiu waweza kuwa wa kiuchumi, kijamii, kijinsia, kimsimamo, kifikra au kimawazo.
Kwenye hadithi ya Mke Wangu, utabaka unajitokeza pale tunapodhihirishiwa utajiri wa wavyele wa msimulizi na wakati uo huo tunadhihirishiwa ufukara wa wahusika wengine kama bazazi wa madafu. Maisha ya bazazi wa madafu nay a msimulizi yanatupa taswra kamili ya utabaka wa kijamii.
Utengano wa kifikra pia unajitokeza kati ya msimulizi na mkewe. Wawili hawa wanaakilisha misimamo pinzani kati ya fikra za jadi na zile za kisasa.

4. Ndoa
Ndoa ni makubaliano rasmi kati ya mume na mke ya kuishi pamoja.
Ndoa zinazotajwa hadithini ni zile za wazazi.
Ndoa zilizotajwa hadithini ni mbili. Kwanza, ipo ndoa kati ya msimulizi na Aziza. Ya pili ni ndoa kati ya wazazi wa msimulizi.
Ndoa kati ya msimulizi na Aziza inakumbwa na matatizo si haba. Matatizo haya yanachimbuka kutokana na ubaidi wa malezi ya wachumba hawa. Huku msimulizi umuhimu wa vyombo na mienendo ya kisasa, Aziza anasisitiza kuwa mila, desturi na vyombo vya jadi ni lazima vitekelezwe. Ndoa hii inaishia kwa Aziza kumwomba mumewe talaka.
Mwishoni mwa hadithi tunaashiriwa ndoa mpya kati ya aziza na bazazi wa madafu.
Hatuelezwi sana kuhusu ndoa kati ya wazazi wa msimulizi. Hata hivyo ndoa hii inaweza kuelezwa kama ndoa inayoongozwa na kaida za jadi. Hii ni kwa sababu wanamuongoza msimulizi kumuoa mke anayefwata kaida za jadi.

5. Taasubi ya kiume na matatizo yanayowakumba wanawake
Taasubi ya kiume ni mfumo wa kijamii ambamo mwanamume hupewa nafasi ya juu kumliko mwanamume. Kwenye mfumo kama huu, mwanamume hukumbwa na matatizo si haba.
Jamii ya mke wangu inaweza kuelezwa kama inayoongozwa na mfumo huu.
Msimulizi anabainisha taasubi ya kiume pale ambapo anawalaumu wanawake kwa matatizo yote yanayokumba ndoa. Anapomwona Fedhele na wanaume, anamlaumu fedhele pekee yake na kuwapuuzilia mbali wale wanaume.
Isitoshe, msimulizi anawadharau wanawake na kuwalinganisha na watoto.
Aidha, msimulizi anamlinganisha mkewe na tunda linalostahili kuvimbikwa ili live.
Hata hivyo, japo Aziza ni mwanamke wa shamba, anajitokeza kama mwanamke aliyejikomboa kimawazo na mwenye hekima tele.

6. Ukengeushi
Ukengeushi ni hali ya mtu kwenda kando na uhalisia wa kijamii. Msimulizi, Fedhele Salma na Seluwa ni baadhi ya wahusika ambao wamekengeuka. Maisha yao hayaingiliani na uhalisia wa mazingira yao.
Japo, fedhele na salma wanajipaka marangi kwa azma ya kuonyesha kuwa wamezinduka, tabia hii inawaudhi wanajamii akiwemo msimulizi. Aidha, tabia ya Fedhele ya kutembea usiku na wanaume inamuharibia sifa mbele ya msimulizi.
Msimulizi naye ni mhusika mwingine aliyekengeuka, licha ya kuwa yeye ni msomi aliyefikia kileleta. Anapigwa chenga na hekima ya msichana wa shamba. Aziza anamdhihirishia kuwa elimu yake haikumfaa kwa lolote bali imechangia kumfumba macho ili asiung’amue uhalisia wa kijamii.
Maswali
Eleza namna maudhui yafwatayo yalivyoendelezwa kwenye hadithi ya Mke Wangu;
i) Ndoa
ii) Utabaka
iii) Elimu
iv) Ukengeushi
5. MATUMIZI YA LUGHA
Zifwatazo ni baadhi ya mbinu za kisanaa na mbinu za lugha zilizotumiwa kwenye hadithi.
MBINU ZA KISANAA ni mbinu zote zinabuniwa na kutumiwa na msanii kuupitisha ujumbe wake. Hizi ni pamoja na usimulizi, taswira, virejeshi nyuma, maswali balagha, sadfa, chuku, kinaya, hadithi ndani ya hadithi.
MBINU ZA LUGHA pia huitwa tamathali za usemi. Ni matumizi ya vipengele vya lugha vya kimapokeo kama vile methali, nahau, vitendawili, tanakali za sauti, istiari na tashbihi.
1. Usimulizi uliotumiwa kwenye hadithi ni wa nafsi ya kwanza.
Msimulizi ni mmoja wa wahusika.
Anatusimulia alivyozaliwa na wakwasi, akasoma hadi viwango vya juu na akachaguliwa mke wa shamba na wazazi wake.
Anaendelea kutusimulia kadhia zinazoikumba aila yake na migogoro inayoibuka kati yake na mkewe.
2. Taswira mbalimbali zinajitokeza kwenye hadithi ya Mke Wangu. Taswira ni picha zinazochoreka mawazoni tunapozisoma kazi za fasihi. Pia huitwa jazanda.
Kutokana na maelezo ya msimulizi, tunapata picha kamili ya Salma, Fedhele na Seluwa. Fedhele na Salma wanachoreka mawazoni mwetu kama wasichana waliojirema na kujipodoa kwa mapambo ya kisasa. Katika ukurasa wa 18, Fedhele anaelezwa kama msichana aliiyevalia kanzu fupi na Salma kama mwenye kujipaka marangi.
Mbali na kuwa mwenye kidomo, Seluwa anachorwa kama msichana mwenye kujipodoa, msichana mcheshi na mwingi wa usasa.
Swali:
Eleza picha inayokujia mawazoni;
Kumhusu msimulizi, Aziza na bazazi wa madafu.
Kuhusu mikono ya msimulizi na nyayo za Aziza.
3. Hadithi inaanza kwa kirejeshi nyuma. Tunarejeshwa hadi enzi ambazo msimulizi alichaguliwa mke na ninaye. Kirejeshi nyuma hiki ni muhimu katika kuielewa hadithi hii maana kinatupa usuli wa hadithi. Kirejeshi nyuma hiki kinatufafanulia maswala ambayo ni msingi wa migogoro inayoibuka hadithini. Matatizo yanayoikumba familia ya msimulizi yanatokana na vigezo vibovu vilivyotumiwa katika kumchagulia msimulizi mke.
4. Maswali balagha:
… si lazima kwa hivyo, Aziza awe mwepesi, msikivu, mwelekevu? (uk 18) msimulizi anatumia swali hili kueleza kuwa maadam Aziza kakulia shamba, ni lazima hana jambo. Kwenye ukurasa wa 19, Aziza anatumia maswali balagha kumbeza msimulizi, anauliza;
Mimi nilikuwa nikitazamia nitaolewa na nani katika dunia hii? …nitapata mume au gumegune tu kama wewe? …basi wewe ndiye mume wa kunioa miye, we? …huoni wewe wala hupimi?
Katika mazungumzo yake na msimulizi, Aziza anadhihirisha utumizi wa maswali balagha, taja na ufafanue umuhimu wa maswali balagha katika maongezi ya msimulizi. (katika kulijibu swali hili, mwanafunzi atafute na kutaja mifano zaidi ya maswali balagha kwenye hadithi)
5. Sadfa ni mbinu ya kisanaa ambapo mambo mawili yanatokea kwa pamoja bila kupangwa. Inasadifu kuwa siku ambayo Seluwa alimgeni msimulizi na kumwamkua kwa kumwingia maungoni, bazazi wa madafu anapita akinadi madafu, hapo hapo Aziz anamwita ukumbini, anaomba talaka kutoka kwa msimulizi na kumtaja bazazi wa madafu kama mume wake.

6. Chuku: ni mbinu ya kisanii inayoeleza jambo kwa namna iliyotiwa chumvi. Katika kuisifia nyayo za miguu yake, Aziza anadai kuwa miguu yake haidungiki kwa miiba. Kwamba hata ukiushindilia mwiba kwenye nyayo zake, mwiba utavunjika!
7. Kinaya: ni kinaya kuwa msimulizi anayepanga kumchanua Aziza anachanuliwa na Aziza.
8. Hadithi ndani ya hadithi: kwenye hadithi ya Mke Wangu, msimulizi anaiwazia hadithi ya Nunez ambaye alikuwa chongo na akafikiria kuwa angekuwa mfalme wa vipofu. Hadithi hii inatusaidia kuelewa ung’amuzi wa msimulizi kuwa utamaduni wake na ule wa aziza haungeingiana.
9. Methali

10. Nahau na misemo iliyotumiwa hadithini ni pamoja na;
Elekeza rohoni (uk. 18) inayomaanisha kumpenda mtu.
Weka kando inayomaanisha kupuuza
Mtoto mbichi ni msemo wenye maana ya motto mchanga
Tia mguu mjini: pata kufika mjini
Kumvinya mwari: kumwelekeza mtu kwa njia unayotaka wewe
Madarasa: mafunzo
Toa macho: kodoa macho
Zawadi za vicheko: kuchekeshwa
Kumtoa kinyanyaa: kumzindua mtu na kumtoa ushamba

11. Tanakali za sauti: aliondoka nyatunyatu
12. Istiara/ istiari
13. Tashbihi: … kama mtoto anavyonyonya:
…wanawake ni kama watoto wadogo: hii ni kauli ya msimulizi inayotubainishia mtazamo wa msimulizi kuwahusu wanawake.
…ngozi imekacha utafikiri msasa: msimulizi anatumia tashbihi hii kuueleza mkono wa Aziza.

Mwongozo wa Damu Nyeusi Part 2

SAMAKI WA NCHI ZA JOTO

 

Hadithi hii anaanzi wakati ambapo wahusika Zac na Christine wamo chumbani mwa Zac wakipga gumzo. Chumba hicho kilikuwa na picha ya bob marley ilityorarukararuka juu ya dawati la zac

Pindi tu Peter ambaye ni rafikiye Zac aliingia. Peter alikuwa muuza samaki wan chi za Joto nje ya nchi hii. Christine alitabasamu kwa geresha alipomona Peter aliyeonekena kuvutiwa na chumba uchwara cha Zac. Zac aliyependa sana kuongea kama Mmarekani,alimkaribisha Peter kitini lakini alikataa kukikalia alikalia kitanda ambapo Christine alikuwa ameketi, Christne alijivuta mbali naye.

Zac alimwelezea Peter kuwa Christine ni rafiki ya na akawaletea vinywaji. Wakati huo alivunja kimya kilichokuwa chumbani humo na kumwongelesha Christine. Alimuuliza kosi aliyokuwa anasomea naye akajibu akiwa ametabasamu. Baada ya muda mfupi Zac alirudi nyumbani na Christine akamaliza kinywaji chake na kuwaaga alipokuwa njiani alikashifu nafsi yake mbona hakusema jambo lolote la maana.

Mwishoni mwa juma Zac alimwambia Christine kwamba Peter angetaka amtembelee tena kwani alipendezwa naye na pia anaweza enda na rafikiye Miriam Peter aliishi huko Tank hill.

Siku ilipowaadia Peter aliwaandalia vinywaji huku wakipga gumzo walitazama video ya ‘Karate kid’. Pindi tu video iliisha Miriam aliongozwa katika chumba cha wageni naye Christine akapelekwa chumbani mwa Peter na Zac akabaki kochini.

Naye Christine akawa na mazoea ya kwenda Tank Hill. Dadake Christine Dorothy alimwonya Christine kuhusu uhusiano wake na Peter lakini aliipuuza mawaidha ya dadake.

Christine alitaka kujua jina la pili la Peter lakini alikataa kumwambia kwani alitaka kuheshimiwa huko Afrika, Baadaye alitambua kwamba jina lake ni Smithson na alitoka tabaka la chini la wazungu.

Siku moja Peter alimpigia simu Christine aende kwake na alipowasili walianza burudani na baadaye alijipata kitandani mwa Peter . Baada ya miezi Christine aligundua kwamba ni mja mzito na alijua kwamba kama angemwambia Peter hangefanya lolote na kasha akaamua kuavya mimba. Christine alienda kumweleza Peter,lakini wote hawakutaka mtoto. Christine alitabiri gari iliyokuwa na muziki wenye mapigo ya juu na kuelekea nyumbani.

 

WAHUSIKA

 • Christine/ msimulizi
 • Zac
 • Peter
 • Deogracias na Wafanyakazi wa Peter
 • Miriam
 • Dorothy
 • Margaret
 • Jagjit na Sunjah Patel

 

CHRISTINE

Ni msimulizi wa hadithi ya Samaki wa Nchi za Joto. Ni msichana wa wa umri wa miaka ishirini anayesomea Sosholojia katika chuo Kikuu cha Makerere.

Anadhihirika kama mwenye sif zifwatazo;

Kwanza ni msichana msomi kwa sababu tunaelezwa kuwa alisoma hadi Chuo Kikuu. Zac anamueleza Peter kuwa Christine ndiye msichana mrembo zaidi pale chuoni.

Christine anajitokeza kama mdadisi wa mambo, anamchuja Peter na kumuumbua kimaumbile. Anadadisi na kuelewa kuwa Peter alipata faida kubwa kutokana na biashara ya samaki. Samaki ambao anadai kuwa wanarejeshwa na kuuzwa katika maduka ya nyama pendwa. Anang’amua kuwa Peter na Zac walifanya biashara ya bangi.

Kila mara, anaichuja nafsi yake na kujiuliza maswali, anajishutumu kwa kutomwambia Peter jambo la maana. Anayachuja maneno na matendo ya watu kwa makini. Anajihakiki na kuyahakiki matendo yake. Anaigundua japo anaikwepa hali yake ya umaaskini, kudhulumiwa na kudharauliwa na Peter.

Ni mwepesi wa kushawishika. Kutokana na udhaifu huu, Christine anajiingiza katika uhusiano na Peter. Anashawishika kwa haraka kuandamana na Zac hadi kwa Peter. Anashawishiwa na Margaret kuavya mimba. Kutokana na udhaifu huu, anatumiwa na kutupwa.

Unuhimu wa Christine

Ni kielelezo cha wasichana wenye elimu na wajihi lakini wanaoponzwa na ulimwengu kutokana na umaskini na tama.

Isitoshe, Christine anawakilisha dhulma inayofanyiwa wanawake na waafrika kwa ujumla.

Ni kana kwamba mwaandishi anamtumia Christine kutuonya dhidi ya kujiingiza katika uhusiano wa kimapenzi kiholela bila ya kizisikiliza nathari zetu. Matendo na hatma ya Christine inadhihirisha ukweli wa methali, ‘Enga kabla ya kulenga’ / ‘Tahadhari kabla ya hatari’ / ‘Usipoziba ufa utajenga ukuta’ na nyingine nyingi zenye maana sawa na hiyo

Hatimaye, baada yake kutumiwa na kutupwa na Peter, Christine anaamua kurjea kwao pengine akiongozwa na imani kuwa, ‘Mwenda tezi na omo, marejeo ni ngamani’

Maisha ya Christine yanatudhihirishia namna wazungu wanapozitumia raslimali za Afrika na kuzizorotesha kabla ya kuzitupilia mbali.

 

 

 

ZAC

Ni mwanachuo mwenza wa Christine, hivi tunaweza sema kuwa yeye ni msomi. Aidha, Peter ni mwenye bidii kwa sababu tunaelezwa kuwa wakati wa likizo, yeye alikuwa akifanya kazi katika kampuni ya Peter.

Anaelezwa na Christine kama kijana aliye na uhalisia, kwamba tofauti na vijana wengine, Zac hakuwa na ndoto za kiuwendawazimu za kuwa watu wakubwa maishani.

Zac anajitokeza kama mwaafrika aliyekengeuka. Anajidhihirisha kama mwafrika anayeiga kuzungumza kwa wamarekani.

Zac ni mshawishi na ndiyo sababu anatumiwa na Peter ili kumshawishi Christine akubali kwenda Tank Hill. Katika ushawishi huu, anajitokeza kama mpenda anasa, anamwambia Christine; … utafurahia matembezi hayo sana, patakuwa na vinywaji vyakula tele na video… (uk 30)

Pia, Zac anajitokeza kama kijana mlevi kwa sababu anapokuwa nyumbani mwa Peter, analewa na kuanza kubwabwaja.

Shughuli zake na Peter zinamdhihirisha kama kijana msiri kwa sababu anajihusisha na shughuli za kuuza bangi bila kutuhumiwa na yeyote.

Umuhimu wa Zac

Zac ni kielelezo cha cha waafrika vibaraka wanaoiga mienendo ya kimagharibi bila kuichuja. Pia, anawaakilisha wafrika wachache wanaotumiwa na wageni kulichafua bara la Afrika kupitia kwa dawa za kulevya na usherati. Zac ni wakala wa peter anayetumiwa kuyapenyeza maovu barani.

Kupitia kwa mhusika Zac, maudhui ya ukoloni mamboleo, ukengeushi, umaskini, usaliti na matumizi ya dawa za kulevya yanaelezeaka.

PETER

Huyu ni mwanamume wa kizungu mwenye umri wa yapata miaka thelathini na tano. Yeye ni mlanguzi wa dawa za kulevya japo anajificha katika biashara ya ununuzi na uuzaji wa samaki. Hivyo anaweza kuelezwa kama mnafiki. Unafiki wake pia unajitokeza pale anapozungumza na Christine kwa upole wakiwa katika chumba cha Zac, (uk 29) upole huu unatoweka pindi tu anapotua mguu afisini pake.

Aidha, Peter ana madharau kwa waafrika. Anawadharau kwa kutoiandika busara inayodaiwa kuibwa kutoka Misri. Anadharau desturi za waafrika na kumbusu Christine shavuni tena kadamnasi ya watu. Pia, anawapa wafanyakazi wake kazi ngumu na kuwaamuru kama nyapara.

Umuhimu wa Peter

Peter ametumiwa kuendeleza maudhui ya ukoloni mamboleo yeye ni mzungu anayeendeleza uozo katika jamii ya kiafrika; Anapunja raslimali ya Afrika kama vile samaki. Anachangia matumizi ya dawa za kulevya, anawaingiza vijana katika ulevi na anasa huku akiwafanya wasahau masomo yao, anawatumia wasichana waafrika kimapenzi na kuwatupa pindi anapomaliza kukidhi haja yake. Isitoshe anahujumu uchumi wa nchi kwa kushiriki biashara ya magendo ya kuuza na kununua sarafu.

Kwa ujumla, matendo ya Peter yanazorotesha uchumi na maadili ya Afrika.

Shughuli zake ni kioo cha kutuonyesha chanzo cha umaskini, upotovu wa kimaadili na unyonge wa watu wa Afrika.

Kupitia kwa mhusika Peter, tunang’amua ukweli wa methali kuwa, ‘vyote ving’aavyo si dhahabu’

DEOGRACIAS NA WAFANYAKAZI WENGINE WA PETER

Deogracias ni mfanyakazi wa Peter wa nyumbani. Mbali naye, pana wafanyakazi wengine afisini pa Peter.

Kwa jumla, wafanyakazi wa Peter ni watiifu, wanamhudumia bwana wao vyema. Aidha, wafanyakazi wa Peter ni waoga. Deogacias anauvumilia uovu utendwao na Peter kwa wasichana wa kiafrika badala ya kuulani. Wafanyakazi wengine wanajitia kufanya kazi Peter anapowatazama.

Umuhimu wa wafanyakazi wa Peter

Wafanyakazi hawa wanaashiria unyonge wa mwaafrika. Unyonge huu umetokana na kubebeshwa mzigo mzito wa kuwatumikia mabwana wa kizungu. Inahuzunisha kuwa wafanyakazi hawa hawafanyi juhudi zozote za kujikomboa.

MIRIAM

Na rafikiye Christine, anaelezeka kama msichana mrembo. Anaelezwa na Christine kama msichana mrefu na mwembamba, mwenye macho ya vikombe Aidha, Miriam ana ujasiri wa kuvuta sigara na kulewa kadamnasi ya watu. Kwa mintarafu hii basi tunaweza kuhitimisha kuwa Miriam amepotoka kimaadili. Utovu wake wa nidhamu unaendelea kudhihirika wakati ambapo yeye pamoja na Margaret wanaunga mkono azma ya Christine ya kuavya mimba

Ulevi wa Miriam unadhihiriika waziwazi wanapomgeni Peter. Analewa na kuanza kucheka sebuleni kivoloya.

Umuhimu wa Miriam

Miriam anawakilisha wasomi waliopotoka kimaadili kwa kujihusisha na uhuni kama vile uvutaji sigara, ulevi na uavyaji mimba.

DOROTHY

Huyu ni dadake Christine mkubwa. Anaelezwa kama mlokole, …Dorothy alikuwa mkristu aliyeokoka…(uk. 31)

Licha ya kuwa mkubwa wa Christine, anakosa ujasiri wa kumkanya mnunawe dhidii ya kuhusiana na Peter. Badala yake, Dorothy anadai kuwa aliota Christine akipewa sumu na wazungu.

Umuhimu wa Dorothy

Kupitia kwa Dorothy, tunapata kufahamu madhara ya kutolikabili tatizo kwa ujasiri. Dorothy ni kielelezo cha jamaa walioshindwa kutekeleza wajibu wa kuwashauri wadogo zao.

MARGARET

Ni dadake Miriam anayefanya kazi ya uuguzi katika zahanati moja jiijini. Utovu wake wa maadili unajitokeza pale anamuunga mkono Christine kuavya mimba. Anaitumia taaluma yake vibaya kuwasaidia wasichana kuavya mimba.

Umuhimu wa Margaret

Anawakilisha wataalamu waliopotoka kimaadili na wanaoongozwa na tama huku wakishirikiana kufanya maovu kama vile uavyaji mimba

JAGJIT NA SUNJAH PATEL

Hawa ni wahindi waliofanya biashara ya magendo na Peter. Mbali na kuwa wajanja wa kufanya biashara ya magendo, wawili hawa nii watu laghai kwa kuwa wanapania kumuuzia Peter noti bandia

Umuhimu wa Jagjit na Sunjah

Hawa wametumiwa kama wahusika wajenzi kwa sababu wanaijenga tabia ya kiulaghai ya Peter. Pamoja na Peter, wanaendeleza hujma dhidi ya uchumi wa nchi.

MASWALI

‘Msimulizi hampendi Peter kwa dhati’, jadili ukirejelea hadithi fupi ya Samaki wa Nchi za Joto.

Jadili uhusika wa Miriam, Dorothy na Margaret katika ujenzi wa wahusika wakuu kwenye hadithi.

DHAMIRA

Yamkini hadithi imelenga kujadili uovu unaoingizwa katika nchi za bara la Afrika na wazungu. Uovu huu ni pamoja na ulevi, ukahaba, ulanguzi wa dawa za kulevya, biashara ya magendo na ukahaba. Azma hii mbi inachangiwa na uwepo wa waafrika wasaliti kama Zac, waoga kama wafanyakazi wa Peter, wasio na msimamo thabiti kama Christine na wale wasio na ukakamavu kama Dorothy.

Margaret na mtaalamu wa unusukaputi ni baadhi ya wataalamu ambao wanatumia maarifa yao na taluma zao kuangamiza jamii badala ya kuiimarisha.

Msimamo wa mwandishi; Japo mwandishi anaelekea kuyahusisha matatizo ya Afrika na wageni, anasisitiza mchango wa waafrika wenyewe katika kujizorotesha.

 

 

MASWALI

Je,ni nini suala kuu katika hadithi?

MAUDHUI

Mafunzo yafwatayo yanajitokeza katika hadithi fupi ya Samaki wa Nchi za Joto

Ukoloni mamboleo; Peter anawafanyisha kazi wafanyakazi wake naa kuwatolea amri kama nyapara. Aidha, anawanyanyasa wasichana wa kiafrika kimapenzi.

Aidha biashara ya Peter ya samaki ni ya kujinufaisha yeye binafsi huku akiwapunja waafrika.

Pia, anawatumia vijana kama Zac kwa manufaa yake ya kibinafsi

Usaliti; Zac anausaliti urafiki wake na Christine kwa kumuongoza kuingia katika urafiki na Peter. Licha ya kujua tabia za Peter, Zac anamshawishi Christine kuingia katika urafiki naye.

Vilevile, Christine anazisaliti hisia zake. Ni bayana kuwa hisia za Chrisine zinamuonya dhidi ya kujiingiza katika urafiki na Peter. Hata hivyo anazipuuza na kujitia katika urafiki uliomsababishia madhara tele.

Mapenzi; mapenzi yanayojitokeza katika hadithi yametawaliwa na unafiki na usaliti.

Zac anajifanya rafiki wa Christine lakini hatimaye anamsaliti kwa kumtaka ashiriki mapenzi na Peter.

Peter naye ana mapenzi ya uongo kwa Christine. Anajifanya kama mwenye kumjali lakini Christine anaposhika mimba na kuavya anampuuza na kumtupa. Inaelekea kuwa alimpenda tu kwa muda ili kukidhi haja yake ya muda.

Yamkini Christina naye anampenda Peter kutokana na dhifa kedekede alizoandaliwa pamoja na zawadi mbalimbali alizompa.

Ulanguzi na Matumizi ya dawa za kulevya; maudhui haya yanaendelezwa na Peter pamoja na Zac. Tunaelezwa kuwa Zac alimtafutia Peter bangi.

Ukengeushi; huku ni kupotoka na kutenda mmbo kinyume na matarajio ya jamii. Zac ndiye mhusika aliyekengeuka sana.

Anajitia kutaka kuzungumza kama mmarekani mweusi. Pia, hataki kuzungumza Kiganda na Deogracias, badala yake, yeye anazungumza Kiingereza.

Tabia ya Miriam kulewa na kuvuta sigara kadamnasi ya watu haitarajiwi katika jamii ya Afrika.

Aidha, suala la kupigana busu hadharani halikubaliwi na jamii ya afrika. Hivi basi, Christine anakengeushwa na mienendo ya Peter ya kumbusu hadharani.

MASWALI

Eleza namna maudhui

Utabaka, Elimu, Ubarakala na ulaghai, Matatizo ya wanawake

 

 

DAMU NYEUSI

Ni hadithi inayomhusu Fikirini ambaye ni mwanafunzi wa shahada ya Uzamifu aliyeenda kusomea Marekani. Huko uzunguni anakutana na changamoto za kubaguliwa kwa rangi ya na wazungu na weusi wenzake.

Hadithi iaanzapo anaachwa na basi ambalo linaendeshwa na mzungu kwa kushukiwa kuwa jambazi. Hatimaye anakumbuka alivyofikishwa mahakamani na kupigwa faini baada ya kuitwa plisi na mwanamke mzungu aliposahau kufunga zipu ya suruali yak. Aliona kwamba kama angekuwa Afrika,ndugu zake wangemfanyia hisani badala ya kumwitaia polisi. Jaji mweusi alimtoza faini ya dola mia mbili na kuepuka kifungo cha miezi sita gerezani.

Baadaye alipokuwa akitembea kuelekea shuleni,alipatana na mwanamke mweusi ambaye alimwalika nyumbani mwake. Fikirini hakujua nia yake lakini mwanamke huyo alikuwa amemweleza kuwa atampeleka hadi chuoni lakini kwanza waingie nyumbani mwake.Wakiwa humo ndani, ndugu yake mwanamke huyo aliufunga mlango.Fiona alianza kumwitisha pesa alizo nazo lakini hakuwa nazo. Alijaribu kutoroka alipohisi kwamba yumo hatarini lakini Fiona alimwita Bob na kumweleza kwamba Fikirini alikuwa anajaribu kumbaka. Bob alimwambia Fikirini auwachilie mkoba wake naye Fiona kamwambia avue nguo zote. Baada ya kuchakurachakura mifuko yake na kupata hamna kitu, Bob alimwachilia na kumwambia asirudi huko tena. Fiona alikataa aachiliwe na kudai kuwa angetaka kumuua. Hatimaye, Fikirini aliachiliwa huru akiwa tupu na akakimbia kama mtu aliyepagawa.

Ijapokuwa Fikirini aliviacha vitu vyake nyuma,kama vitambulisho,alimshukuru Mungu kwa kumwachia uhai wake.

DHAMIRA

Mwandishi anazungumzia kuhusu ubaguzi kati ya wazungu na weusi na pia weusi na weusi. Dhamira ni kuwa mwandishi anakashifu swala la ubaguzi wa rangi.

MAUDHUI

1.UBAGUZI WA RANGI.

Watu wenye rangi nyeusi wanabaguliwa na wazungu au weusi wenzao.Anabaguliwa barabarani kuwa yeye ni jambazi.

Pia chuoni anabaguliwa.Anapewa alama chache ingawa anafanya vizuri katika mtihani. Weusi wenzaka wanabagua kwa vile ametoka Afrika na ameenda kuwaharibia.

2.ELIMU.

Fikirini alienda huko kutafuta elimu ambapo alikuwa anasomea shahada ya uzamiifu.

3.UJAMBAZI

Fikirini alikutana na majambazi wawili aliowaita ndugu zake lakini walimvamia na kumtupa nje akiwa tupu.

4.UVUMILIVU.

Fikirini aliweza kuvumilia matatizo mengi kama ubaguzi ili awezekumaliza masomo yake na kurejea nyumbani.

5.USALITI.

“Dadake” Fikirini aliisaliti imani yake kwa kumhadaa.

6.UKATILI.

“Dadake” Fikirini alikuwa anataka kummaliza Fikirini kwa sababu ya kukosa pesa.

7.UNAFIKI.

Huyo “dadake” alijifanya mwema ili amsaidie Fikirini lakini alikuwa na nia yake.

1.FIKIRINI.

Ni mwanafunzi na ametoka katika nchi za Afrika.

SIFA

 • Ni mvumilivu,amevumilia ubaguzi;baridi na dhuluma
 • Ni msomi,alienda uingereza ili aweze kumalizia masomo yake ya shahada
 • Ni mwoga,alijisaidia aliposhikwa na woga
 • Mwenye imani,aliamini kwamba Fiona angeweza kumsaidia kwa gari lake nzee ili ampeleke chuoni.
 • Mpole,alipoulizwa maswali ya upuzi wenzake alivumilia
 • Mwenye bahati mbaya (mdubira),alisahau kufunga zipu ,alipatana na majambazi.
 • Mjinga,aliamini kwa haraka kwamba “dadake” angemsaidia.
 • Mzalendo,aliipenda nchi yake.

 

2.WAZUNGU.

SIFA

 • Ni wenye ubaguzi mwingi .
 • Ni wenye imani potovu,wanaamini kwamba Waafrika ni kama nyani.

3.FIONA NA BOB.

Ni wamarekani weusi.

 • SIFA
 • Ni majambazi.
 • Ni wakatili,badala ya kumsaidia mtu akiwa na shida wanazidisha
 • Fiona ni mnafiki,alijifanya kumsaidia Fikirini ila ana zake.

MTINDO

1.USIMULIZI

Masimulizi ya mwandishi yanatumia nafsi ya tatu

2.KUCHANGANYA NDIMI.

Fikirini aliulizwa“Do youspeak English?”“ someone called to say you are exposing yourself.”

“How you doing?”                                                                                                                                                                                                                                     “Am cool”                                                                                                                                                                                                        “I say remove your clothes or else”                                                                                                                                                                              “ I say shoot him Bob”

 

 

MATUMIZI YA LUGHA.

1.METHALI.

 • Nyumbani ni nyumbani ingawa ni pangoni – Ilitumiwa na Fikrini alipokuwa akirejelea kwao nyumbani ambako ni Afrika naye ako uingereza ambako ni kuzurui kuliko kwao lakini hata kama kwao si kuzuri ivo ni nyumbani.
 • Baharia wa pemba hufa maji mazoea – mabaharia wa Pemba wamezoea kufa mali na ni jambo la kawaida.
 • Simba akikosa nyama hukula nyasi – Fikirini alikosa chakula kizuri cha kukula kwa hivyo alilizimishwa kula chakula chao.
 • Siku ya kufa nyani miti yote huteleza – Siku ya mkosi ni mkosi na hakuna jinsi ambavyo mtu anaweza kuepuka.

2. TANAKALI ZA SAUTI

Pepesuka pepesu pepesu.

 • Nyapia nyapu nyapu
 • Nyeupe pepepe

3.MISEMO

 

 • Mlevi chakari – mtu aliyelewa kupindukia .
 • Maji yamezidi unga – mambo kuzidi matarajio
 • Kusalimu amri – kukubali.
 • Kufa ganzi – kupoteza fahamu
 • Elewa fika.

Mwogozo Wa Damu Nyeusi Part 3

GILASI YA MWISHO MAKABURINI

Katika hadithi hii tunapatana na Msoi mwenye utambuzi wa kipekee ya mamabo yatakayotokea. Msoi alipata hisia flani yenye kitisho na wasiwasi. Ndoto nyingi ambazo Msoi aliwahi kuota mara mara hua ingawa marafiki wake hawakuamini.

Hisia hizo ambazo Msoi alijaribu kuepuka kwa muda kwa mwezi mmoja hatimaye zilimfanya awe mwoga zaidi yeye pamoja na marafi zake walikuwa wanaenda katika bar iliyokuwa kwenye maskani ya mava ili kunywa na kujiburudisha baada ya kazi. Pia pahali hapo palipopachikwa jina la kimombo exotic resort.

Siku moja aliamua kutoenda katika mava kwani hisia zake zilimfanya aogope sana. Kwa sababu aliona kwamba balaa kubwa itatokea,Semkwa rafikiye Msoi alienda kwake nyumbani ili kumsihi waende katika mava akaitikia shingo upande. Walipokuwa wakitokea Msoi aliligonga bakuli la maua likavunjika vipande vipande ,alikuwa karibu kuanguka akiteremsha mguu na pia alijibana kidole kidogo kwenye mlango wa gari. Hizi zilikuwa ishara za kuonyesha kwamba jambo mbaya litatendeka.

Njiani walisikia mgurumo wa radi ambayo Semkwa aliona kuwa jambo la kawaida. Walipofika kwenye daa ya makaburini,walipatana na Asha na Josefina. Walipokaa chini,Msoi aligeuza namna yake ya kukaa. Siku hiyo alitaka kuyaangalia mava ili jambo likitokea ataweza kutoroka.

Muda ulivyozidi kuyoyoma , Msoi na marafiki wake walijiburudisha na vinywaji na muziki uliochezwa na bendi. Asha na Msoi walipokuwa wakichheza densi, Msoi alionekana mwenye wasiwasi. Wenzake wakaanza kumtani hadi ikambidi anyamaze ili angoje kile ambacho kitaendeea. Msoi alingwa na kuburudika nao ijapokuwa walimtani na kumkejeli kuhusu ndoto zake. Asha aliburudishwa na Msoi kuhusu matukio yaliyotendeka na Msoi kuhusu matukio yaliyotendeka awali ambayo aliona kama ni ya bure tu. Msoi aliamua kujinyamazia.

Wakati ambao kila mtu alikuwa ameshiba walicheza mziki huku wakiwa kwani hawakutosheka. Baada ya muda mfupi, Msoi aliviona vizuu vimejifufua kwa mtindo wa Thriller wa Micheal Jackson, Asha alipiga uyoe ambao uliskika na kila mtu. Watu walipoona yaliyokuwa yakiendelea walitimua mbio hadi kwao nyumbani. Wengine walianguka na kukanyang’wa

Baada ya Asha na Msoi kufika nyumbani waliskia habari kwenye televisheni kwamba wale vizuu walikuwa majambazi ili waibie Baa ya Makaburini pamoja na wateja wao.kwa mara nyingine marafiki zake Msoi walifahamishwa kwamba wanafaa kumsikiliza.

 • Mwandishi anatuhimiza tusipuuze mambo ambayo tunaonywa na marafiki zetu.

MAUDHUI

 • ANASA NA STAREHE

Tunaona kwamba Msoi na Asha walikuwa wanaenda kwenye baa ya makaburini kujiburudisha baada ya kazi na kulewa kiasi cha kujisahau.

 • UHALIFU

Majambazi walivamia watu na kuwaibia mali yao kwani waligundua kwamba watu huogopa wafu

 • ITIKADI NA USHIRIKINA

Ushirikina ni ile hali ya kuamini nguvu nyingine kuliko mungu

Msoi aliamini kwamba baa iliyokuwa kwenye mandhari ya mava ingevamiwa na watu wasiojulikana

 • URAFIKI NA UTANGAMANO

Akina Semkwa,Msoi,Asha na Josephina waliburudika pamoja na kutengamana.walifanya m ambo pamoja

 • UWOGA

Msoi aliota ndoto ambazo zilimfanya awe mwoga.

WAHUSIKA

1.Msoi.

Ni mtu mwenye kipawa utambuzi wa mambo

SIFA

       I.            Ni mbarazi ,ana mazoea ya kukaa na watu wengine hasa katika baa.

     II.            Ni mshiriki anasa,amekuwa akizuru bar ya makaburini ili kustarehe.

  III.            Ni mpole,hana mambo mengi.

  IV.            Ni mwoga.

    V.            Ni mshirikina,anaamini katika mambo ya ushirikina.

  VI.            Anashawishika kwa urahisi.

2.Semkwa,Asha na Josefina.

I.            Ni wabaraza

II.            Wapenda anasa,kila wikendi walikuwa wanakutana katika baa na kuburudika pamoja.

III.            Wabishi,walibishana na Msoi alipowadokezea kuhusu ndoto yao.

IV.            Weye utani ,wanamtania Msoi anapowaeleza kuhusu ndoto yake.

 

 

3.Majambazi.

I.            Ni watu wabunifu –walivaa kama wafu ili waweze kuwaogofya watu

II.            Ni waoga-hawajitokezi moja kwa moja kukabiliana na watu.

III.            Wahalifu –walijaribu mali ya watu baada ya kuwaibia.

KIKAZA.

Hadithi hii inazungumzia kikaza ambacho ni suruali spesheli. Kikaza hiki kimetumiwa kusimamia uongozi katika jamii. Kikaza ni jazanda inayosimamia uongozi. Hadithi inaanza pale ambapo kuna dalili za mvua kunyesha,lakini Mzee Babu akawafahamisha wanakijiji kwamba haitanyesha. Kwanza wanatekede hawakuamini. Kulikuwa na kikao kwa mzee huyu na miongoni mwa waliohudhuria ni Bi Cherenga almaarufu Bi Cherehani na Bw Pima,Bw Machupa pia alikuwepo(msemaji wa kijiji). Wote walitaka Mzee Babu awafunulie kitendawili.

Washona kikaza ni wananchi wenyewe. Kikaza kilikuwa kimepasuka. Bw Mtajika(kiongozi) alifanya makosa kumwacha Bi Mtajika kukiguza kikaza,kwani yeye siye kiongozi. Mapinduzi ni marekebisho yalihitaji kufanywa. Kulikuwa nia uongozi mbays. Bw Pima alipima kikaza na Bi Cherehani kukishona. Bi Cherehani aliwahimiza wanatekede kwenda kukishona kikaza (kurekebisha makosa na kumtoa Bw Mtajika mamlakani) . Kikaza kilihitaji kushonwa. Bi Cherehani alihakikisha kwamba atapunguza kipimo ili kikaza kikaze. Kikaza (uongozi) ni cha ushirika.

Mwandishi anataka kuonyesha kwamba uongozi ni ushirika.

MAUDHUI

1.UONGOZI

Hadithi hii inaongea kuhusu swala la uongozi.

 

 • Uongozi umewakilishawa na kikaza – “suruali ya ndani”
 • Uongozi hushonwa na wananchi.
 • Uongozi ni ushirika.
 • Uongozi mzuri au mbaya hutokana na mchango wa watu wenyewe
 • Mwandishi pia anaguzia swala la uongozi mbaya
 • Bw Mtajika tunaelezwa kwamba kikaza chake kimeraruka na basi uongozi umeigiza dosari.
 • Bi Mtajika amechangia katika uongoza mbaya.
 • Wanawake walishona kikaza kiliochobana

2.UBINAFSI

Bw Mtajika na wenzake waliochaguliwa waliochaguliwa waliwasahau waliwasahau wenzao waliowachagua kama vile kobe alivyowatendea hadithi yake kuenda angani.

 

 

3.USHIRIKIANO

Kikaza kilishonwa kwa kushirikiana. Katika uongozi, lazima pawepo na ushirikiano wa watu wote.

4. MABADILIKO

Baada ya mambo kugonga mwamba, viongozi wanatolewa mamlakani na kubadili uongozi.

5. USALITI

Bwana mtajika na Bi. Mtajika , anawasaliti wananchi kwa kuongoza vibaya na kutomzuia mkewe kukigusa kikaza.

6. UKARIMU

Babu na wanakijiji ni wakarimu wanapopeana mavuno.

7. KUTOWAJIBIKA

Viongozi hawakuajibika katika uongozi wao.

8. UTABIRI

Babu anatabiri.

 

WAHUSIKA

1.   MZEE BABU

 • Ni mtabiri
 • Mkarimu
 • Mwenye busara . Anawatetea na kuwashauri watu
 • Mbaraza. Anapenda kuingiana na watu.
 • Mtambuzi wa mambo.

2.                       BW. MTAJIKA

Kiongoziwa tekede.

SIFA

 1. Ni mweledi wa kuongea .anapoongea, hawei kubadilisha ukweli kuwa uongo.
 2. Mwenye ubinafsi. Alipopata cheo, aliwasahau wengine.
 3. Ni mwanamme anayetawaliwa na mkewe. Alikua amezidiwa na nguvu za pili.
 4. Msailiti. Amewasaliti wananchi wa Tekede kwa kuwasahau (hadithi ya safar ya mzee kobe kwenda angani. )

 

3.      BI CHEREHANI/ BI CHIRENGA.

 • Mshonaji kikazi.
 • Ni mnyamavu kwani hapendi kuzungumza
 • Ni mwenye soni
 • Mkweli. Hapiti njia mbili. Hafichi mambo.
 • Ni mzalendo .hakwenda ikuliuni peke yake.
 • Mwenye bidii kwani anashona kikaza kama jukumu lake.
 • Mvumilivu. Amevumilia kukemewa na watu.

 

4.     BI MTAJIKA.

Msaliti anakigusa kikaza ingawa anaelewa itikada ya jamii ya wana Tekede inayosema kwamba wa pili hafai kugusa kikaza.

Ni mkoloni kwani anaamua kutawala watu apendavyo yeye.

 

 

5.     WANAKIJIJI

Ni wakarimu.Walimpa babu mavuno waliyoyapata.

Wenye mapinduzi. Watu walizinduka kuhusu uongozina Bw. Mtajika.

Ni wenye ushirikiano.Wanashirikiana kumtoa Bi Mtajika kwenye mamlaka.

Ni wasikivu. Wanamsikiliza babu kwa makini.

Ni wenye utamaduni.Wanatii tamaduni zao.K.m bibi hakustahili kugusa kikaza.

 

 

MBINU ZA LUGHA

 

a)      TASHTITI

Ni mbinu ya kukejeli mtu kwa njia ya kutomuudhi moja kwa moja.

Hadithi ya kobe ni tashtiti murua inayoonyesha ubadhilifu, ukaidi na uogozi mbaya wa Bw. Mtajika. Mzee Babu anawapa watu hadithi badala ya kusema yote aliyoyafanya kombo Bw. Mtajikana adhabu atakayoipata atakaposhushwa madaraka.

Ushonaji wa kikaza vibaya kwa Bi. Cherehani na Bw. Pima pia ni tashtiti. Yaonyesha namna ambavyo wanakijiji wa Tedeke waliomchagua kiongozi aliyefaa.

Msemo wa nyani haoni kundule ni semi linaloeleza upambano na kutojali kwa wanakijijij wa Tekede.

b. FUMBO

Kikaza kimetumika kimafumbo kumaanisha uongozi, upimaji Na kushonwa kwa kikaza ni kumteua na kumtwika majukumu ya uongozi. Kupima na kushona kikaza ina maana ya ushirikiano wa jamii katika kumchagua na kumsimika kiongozi.

Wa pili hakuruhusiwa kushika kikaza ni mke wa kiongozi. Kutanda Kwa mawingu meusi angani kusha kukosa kunyesha ni fumbo inayoeleza dhiki ya waakaazi wa Tekede.

 

c. HADITHI

Hadithi katika hadithi hii inamhusu kobe inayosimuliwa na mzee Mzee Babu. Musiliko wa karamu angani ilimjulisha kobe, ndege na kadhalika. Mzee kobe alifanya ujangili na kudai jina sisi sote.

Kila chakula, kinywaji na starehe zilielekezwa kwake. Ndege walitababika na kuamua kumnyanyanya kobe. Manyoya yao na kobe hakuweza kupaa tena ndio maana gamba la kobelena viraka au mipasuko.

D. MAJAZI

Mbinu za kisanaa.

Baadhi ya wahusika wanapewa majina kulingana na sifa au hulka zao. K.m. Mzee Babu alikuwa mzee kuliko wengine. Bw. Mtajika alitojwa mara kwa mara na kila mtu kwa sababu alikua kiongozi wao. Bw.Machupa pima aliyapima kwa uangalifu alivyowaambiwa wanakijiji.

Bw Machupa hakuwa na msimamo dhabiti hasa kuhusu uongozi wa Bw. Mtajika.

e. TAKRIRI

Baadhi ya kauli zimekaririwa ili kutilia mawazo Fulani mkazo k.m Bw. Cherehani na Bw. Pima walikuwepo kushiriki na kutoa mchango walikuwepo vilevile.

Kitendawili cha kukaza kikazidi kukazaa.

f. TABAINI

Ni kusisitiza mambo kwa kutumia vikarushi. Baadhi ya semi zina dhana ya ukinzani lakini kwa hakika hakuna ukinzani kimaana. K.m si salama si chochote hakuna kilichotaka kinywani.

g. TASHBIHI

Yaliyopita huja kama nguvu za sunami.(uk 45) Machupa hutafuna na kupuliza kama panya.

h. BALAGHA

Hayahitaji majibu.

Anasema nini?

Itakuwaje sisi wawili ndio tuwe najibu?

 

6.     MAEKO

Hadithi inapoanza ni usiku wa manene ambapo Hamduni au Duni anaporejea kwake. Anatoka ulevini kama ilivyokuwa desturi yake. Ni majira ya usiku wa manane. Anaimba wimbo wake wa kawaida ambao mwandishi anaita “taarabu njia.” Kwani alizoea kuuimba akiwa njiani kuelekea kwake.

Jamila mkewe Hamduni anapomsikia mumewe anamka ili kumsubiri. Mwanzoni mumewe anamka ili kumsubiri. Mwanzoni mumewe anaonyesha furaha na bashasha kwa kupokelewa na mkewe. Lakini anageuka na kuwa mjeuri mkewe anapojaribu kumsaidia kupanda ngazi za kuingia kwao puia anampiga mkewe teke kwa kukawia kumpatia chakula.

Mwandishi anasema ghasia na zogolaukorofi wa duni zilidi na kukosesha utulivu katika ndoa yao. Majirani na hata jamaa zake jamila walipoona kipigo kimezidi walimshauri ajiondoe kwenye ndoa hiyo. Hata kuna kifana kwa jina salim aliyoyapitia. Alitaka Jamila amwasi duni halafu angetoroka naye.Alishindwa kuelewa Kwa hakika. Salim alimpenda kwa dhati au alitaka kujinufaisha kutokana na hali yake Jamila.

Kwa sababu ya madhila aliyofanyiwa na mumewe Jamila ya kawaida. Alirauka asubuhi na kutayarisha kiamsha kinywa cha kukata na shoka ambacho alikiagizwa kwa fujo. Kenyoye Duni alimpumbaza mkewe kwa mapenzi yasiyo ya kawaida. Alirauki asubuhi na kutayarisha kiamsha kinywa cha kukata na shoka akakusanya nguo zote chafu na kuziroweka ili azifue baadaye kasha akaenda kumwita mkewe. Alimuomba msamaha mkewe kwa yale yote aliyomtendea kasha wakashebeha.

Baada ya hapa maisha yakawa ni yay ohayo amani na mapenzi kwa muiezi miwili, kufarakana, kuombana msamaha, amani na kadhalika.Hta Jamila mwenyewe alishindwa afanye nini. Lakini kwa kiasi kikubwa aliridhishwa na ndoa yake licha ya matatizo aliyoyapata humo.

DHAMIRA

Watu huvimilia mapato wanayoyapata katika ndio hiyo k.m. jina, pesa, mapenzi na kadhalika.

MAUDHUI

1.     ULEVI

Unywaji pombe kupindukia.

Hamduni alilewa kupita kiasi.Mwandishi anataka kukashifu ulevi.

2.     UVUMILIVU

Jamila amevumilia mateso na majirani wanavumilia kero za hamduni.

3.     DHULMA KATIKA NDOA

Hamdunio anamwacha mkewe na kwenda kulevya.

Kumchapa Jamila akiwa amelevya.

4.     MAEKO

Namna ambavyo mtu (Jamila) amewekwa.

Jamila anavumilia dhulma za ndoa kwa kuwa anapewa pesa, mapenzi, anafanyiwa kazi.

 

WAHUSIKA

 

1.HAMDUNI

Ni mhusika mkuu katika hadithi hii na ni mumewe Jamila.

SIFA

1.     MLEVI

Analewa kila siku

2.     Mwenye fujo

Anampiga mkewe.

3.     Ni mkaidi

Alikanywa kupiga makelele usiku lakini anazidisha.

4.     Ni msumbufu

Aliimba usiku watu wakiwa wamelala.

5.     Ni msanii

Alipenda kuimba.

6.     Ni mwenye majuto

Hujitia makosa ambayo alitenda akiwa amelala.

7.     Ni msahaulifu

Anasahau kwa haraka aliyomfanyia mkewe.

8.     Ni mwenye mapenzi.

Anampenda mkewe.

 

2. JAMILA

Mhusika mkuu ni mkewe Hamduni.

SIFA

 1. Mwanamke mwenye umri mdogo.
 2. Ni mvumilivu. Anavumilia masaibu ya ndoa.
 3. Mwenye mapenzi.
 4. Ni mjinga anaishi katika ndoa kwa sababu ya maeko.
 5. Ni msamehevu anamsamehe mumewe kwa aliyamfanyia.
 6. Ni mwenye kutamani kuishi maisha mazuri.
 7. Mwenye matumaini
 8. Mwenye msimamo thabiti hakutaka kutoka kwa mumewe ingawa alishauri afanye hivyo.

3. SALIM

Ni rafikiye Hamduni.

SIFA

 1. Ni mnafiki. Alimwahidi Jamila amuasi duni ili angeweza kutoroka naye.
 2. Ni mwenye mawaidha ya kupotosha. Anamhimiza Jamila atoke kwa duni ili aepuke kuhapo.
 3. Ni msaliti. Anamtaka Jamila ambaye ni bibiye rafiki yako.
 4. Wanapenda amani
 5. Wanamshauri Jamila.
 6. Ni wavumilivu.

4.WANAKIJIJI

 

 

4.     SELA

Ni mhusika mkuu anasomea shule ya Askofu Timotheo mwanawe mzee Buteli.

A)    Ana utu na huruma. Hakuavya mimba pia alipokutana na Masazu aliyejifanya mgonjwa , alimsaidia.

B)    Ni mkarimu. Anampeleka Masazu kwenye kliniki.

C)    Mwenye mapenzi ya dhati. Anampenda Masazu kwa moyo mmoja anampenda ata baada ya kumpa ua uzito.

 

MBINU ZA SANAA

Ø  NYIMBO

Mwandishi ametumia nyimbo kwa nia ya kuwasilisha ujumbe Fulani kuonyesha hulka ya mhusika.

Wimbo wa kwanza unaimbwa na Hamduni anapotoka ulevini kuonyesha kuwa hakujali walivyosema wasebuleni.

Ø  MAJAZI

Mwandishi amewapa wahusika majina yaliyolingana na sifa au hulka zao.

Jina la duni halisi lilikuwa Hamduni lakini watu walizoea kulifupisha na kuwa Duni ili litamkike kwa urahisi. Jina hili lilimfanya adharauliwe na watu mtaani sebuleni.

Salim alikuwa rafikiya Duni ambaye aliyejitolea kuleta hali ya utulivu katika maisha ya Jamila kwani alijiona salama na bora kuliko Hamduni.

 

MBINU ZA LUGHA.

       I.            KEJELI

Duni mtiribu sababu alizoea kuwaamsha majirani zake kwa nyimbo za kilevi. Duni hakuwa mtiribu, hii ni kejeli kwa sababu aliwaudhi wanakijiji kwa nyimbo zake.

2. METHALI

m.f. tunaambiwa kuwa wenyeji wa Sebleni walitoa maneno ya kumlaani Duni akini yalikuwa ni “ dua la kuku haimpati mwewe” yaani Duni, maanake hakubadilika wa kushughulishwa na hayo.

3. MISEMO

“usiku mkubwa” (uk 66) usiku sana. “ kusafiri kwa mapana na marefu” kusafiri sana. “ mjaliwa laana” mtu aliyelaaniwa.

5.     BALAGHA

Mwisho wa haya utakuwa lini ya Rabi? (uk 67) alijiuliza Jamila hakuwa nalo.

6.     KINAYA

Walimwonea Jamila huruma walisema kuwa huko nje kulikuwa wanaume waungwana na majina na staha zao na ambao wangefanya lolote ili wampate Jamila.

7.     UTOHOZI

Baadhi ya maneno yametoholewa kutoka kizungu ili kuonyesha usasa na pia athari za kizungu kwenye maisha ya wahusika.

k.m: stimu- steam

Kozi- course

Bendeji- bandage

Hai- high

Dii – dear

8.     TASHBIHI

Alimpiga mkewe kama ngoma ya kimanga popote apatapo kuonyesha jinsi Duni alivyimpiga mkewe bila huruma.

9.     TAKRIRI

Maneno na semi au kauli zimarudiwa ili kutilia mkazo wazo Fulani k.m mtiribu.

 

Mwongozo wa Damu Nyeusi Part 4

KANDA LA USUFI

Hadithi inaanza kwa kisengere mbele kwa kurejelea jambo au tukio lililotokea mwishoni mwa hadithi selaha masazu walikuwa wameenda kumchukua motto wao waliyempata wakiwa bado wanafunzi.

Vijana hawa walikutana wakiwa shule ya upili Sela katika shule ya Askofu Timotheo naye Masaru akiwa shule ya Lenga juu. Urafiki wao unakita mizizi na kupeleka sela kupata mimba na kufukuzwa shuleni.

 

DHAMIRA

Mwandishi anataka kuonyesha kuwa mzigo wa mwenzioi huwa mwepesi kwako ilhali ni mzito kwake. Wavulana na wanaume watauona mzigo wa kuwa na mimba kama mwepesi lakini kwa wasichana au wanawake mzito.

 

MAUDHUI

1.     Mapenzi

Sela na Chris ni wapenzi kwani mapenzi yalishamiri baina yao.

2.     Urafiki

Palikuwa na urafiki baina ya Sela na Chris na baadaye wakawa wapenzi.

3.     Usaliti

Usaliti nni kumtendea mtu jambo kinyume na imani yake kwako. Masazu alimsaliti Sela kwa kutowajibika katika kuchukua jukumu la kumwitikia Sela kwani ni mimba yake.

4.     Elimu

Chris na Sela ni wanafunzi na wanacheza na elimu yao kwa kutotilia maanani shuleni.

5.     Majuto

Babake Sela anajuta kumpeleka Sela shule. Sela na Mavazu wanajuta.

6.     Umaskini

Kwa umaskini, Sela hangepata nguo za kuvalisha kadogo(mtoto) kwani alivalishwa matambara.

7.     Kazi

Chris anapomaliza elimu yake, alienda kutafuta kazi.

8.     Ujanja

Chris anatumia ujanja na kumwambia Sela kuwa ni mgonjwa ili amwongeleshe Sela.

9.     Ndoa

Sela na Chris wanapanga kuishi pamoja.

10.Ushawishi

Sela anamshawishi Chris wamwendee motto wake ili upweke uuondoke.

11.Ukatili

Babake Sela anawafukuza mamake na Sela nyumbani.

12.Ushauri

Mwalimu mkuu anawasihi wazazi wa Sela kumtafutia Sela shule.

Wazee wa jamii wanamshauri babake Sela kumrudisha kwa jamii zake.

13.Utu

Sela hakuavya mimba.

Razina halati ya Sela anamlisha kadogo.

Sela na mamake walipokelewa na watu wa karibu.

14.Msamaha

Babake Sela aliwarudisha mamake na Sela.

WAHUSIKA

 

 1. Sela
 2. Masazu
 3. Kadogo
 4. Rozina
 5. Mzee Butali
 6. Bi. Magret
 7. Mama Sela
 8. Sista

Ingawaje aliweza kuendelea na masomo yake katika shule ya kutwa ya hapo karibu na kwao. Baada ya kujifungua alikaa nyumbani kwa miezi mitatu akikitunza kitoto chake. Baadaye alimwachia mamake na kurudi shuleni.

Baada ya masomo yake Masazu, alihamia mjini Dafina kutafuta kibarua, na kupata cha kuvuna mkonge upweke na akaonolea kuwa jambo la busara kama angekuwa na mwana wo, kadogo ili amtoe apweke wakati Masazu akiwa kazini.

Sela na mchumbaye waliamua kumwendea mwanao hadi kule kijijini alimokuwa akikaa na halati ya Sela, walipanga safari yao usiku na ikatokea kuwa kulikuwa na mvua iliyosababisha unyevu na utelezi. Walipokuwa njiani wakirudisha Sela na mtoto mgongoni, aliteleza na kuanguka kwenye mto uliokuwa umefurika na kusombwa na maji pamoja na mwanao kadogo.

Masazu alipoona hivyo alijitosa majini ili kuwaokoa. Hadithi hii inapoishi hajabainika kama Masazu aliweza kuwaokoa . Hadithi hii inapoisha hajabainikakama Masazu aliweza kuwaokoa au labda pia alisombwa na maji. Hadithi inaisha kwa taharuki.

 

MBINU ZA KISANAA

 • Mbinu rejeshi
 • Taharuki
 • Maswali ya balagha
 • Taswira
 • Sadfa

1.    Mbinu rejeshi

Hadithi inahusu kumwiba motto lakini mwandishi atarejesha nyumba vile walivyopatana.

2.    Maswali ya Balagha

Haya ni maswali ambayo hayahitaji majibu. K.m mama Sela aliuliza Masazu, “ huyu si mtoto wetu sisi wawili?”

Bw. Butali aliuliza,” mama gani anayemtazama mwana akigeuka afriti?”

3.    Taswira

Hii ni picha ijengewayo mawazoni. K.m. Masazu anachomeka kidole chake ardhini na kula kiapo cha mapenzi yake kwa Sela.

Masazu akiweka vidonge vya dawa kwa mdomo na kumeza kwa maji.

4.    Taharuki

Mwandishi anatueleza kuwa Masazu anapokula kiaop nakiwiliwili cha Sela kinalengezwa na mengine yaliachiwa yalibaki katika himaya ya maumbile.

5.    Sadfa

Sela na Masazu walikutana bila kutafutana na baadaye kuoana.

Bw. Butali hakutarajia mambo aliyokumbana nayo yafanyike kwake.

 

Christine

MBINU ZA KISANAA

1.Mbinu rejeshi.

-Hadithi inahusu mapenzi ya Sela na Masazu.

-Mwandishi anaturudisha nyuma mahali ambapo Masazu na Sela walikutana.

2.Maswali ya balagha.

-Mamake Sela anamuuliza babake Sela kwani Sela si msiba wao bali wa mamake tu.

-Masazu anauliza Sela kwa nini hakujikinga.

3.Taswira.

-Hii ni picha ya mawazoni.

-Hii inajitokeza ambapo Masazu anakichomeka kidole chake ardhini akiwasilisha kiapo kwa Sela kuwa mapenzi yake ni ya dhati.

4.Taluki.

-Hali ya kutojua kilichotendeka hapo mbeleni.

-Ambalo Sela na mtotowe wanatumbukia majini.

-Wakati ambapo Masazu aliapa kiapo aliyeyusha nafsi ya Sela na hatukwambiwa nini ilitendeka.

5.Sadfa.

-Haya ni mambo ambayo hayakutarajiwa kutendeka.

-Sela na Masazu walioana hata baada ya Masazu kumsaliti.

MBINU ZA LUGHA

 

1.TASHBIHI

Hulinganisha kitu na kingine k.m;

 • Kiwiliwili chake mithili ya mbwa anayekabiliana na chatu macho kwa macho.
 • Ulimwengu wake ulivurugika, akawa kama tiara inayopeperushwa na upepo ikaendaarijoyo.
 • Nafasi kama hiyo hutokea kwa nadra ya jua kupatwa na chui aliyelivizia windo lake na sasa limetokea, akajiandaa.

2. Tashhisi

Sifa ya kukipa kitu chenye hakina uhai( uhaishi)

 • Mambo haya mawili yalielekeaa kuungana kuhujumu mkakati wao.
 • Matone yalitua sehemu yao ya hujuma. Mwandishi arejelea pale ambapo Sela na Masazu walikuwa wamejificha chini ya mwembe.
 • Mabaki yalielekea kutapika wanafunzi wakikena kiume.

 

3.Semi.

 • ….baridi shadidi ya usiku(uk59)ina maana kuwa huo ulikuwa na baridi kali.
 • Alijaribu kuvuta kumbukumbu(uk59)yaani alianza kukumbuka.

4.Methali.

 • Mimba ile ya Masazu ilikuwa kanda la usufi.Methali hii inasema kuwa mzigo wa mwenzio ni kanda la usufi.
 • Uchungu wa mwana aujuaye mzazi.(uk63)

5.Istiara.

 • Nyumbani mwa Butali kuligeuka kuwa jehanamu.
 • Mimba ya Sela inalinganishwa na msiba.
 • Usiku wa giza-kukosa matumaini.

 

 

 

 

 

 

SHAKA YA MAMBO.

Hadithi hii inamhusu msichana wa miaka 29 hivi.Tunampata asubuhi na mapema akiwa mwenye gari la abiria akielekea kazini.Anapata gari limejaa lakini kijana mmoja anamwondokea kiti ili akae,jambo lisilo la kawaida hasa hapa Afrika.Akiwa njiani anawaza mengi kuhusu maisha yake.Anaona kuwa tangu afike Nairobi hajapata yale mambo mawili aliyoyafuata kujifunza usekritari na kuwa na uhuru.

Alikuwa anaishi na mzee Mwinyi na familia yake katika mtaa wa Madaraka Estate alipokuwa amekodisha nyumba.Mzee huyu alimchukua kama mwanawe.Pia alikuwa na rafiki wa kiume aliyeitwa Kamata.Hatimaye anafika kazini,mkahawa uliokuwa katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa J.K.I.A na kuanza kazi.Mkubwa wake Grace hangeweza kushika zamu yake kwa sababu alikuwa na miadi yake lakini angemlipa baadaye.Kamata alifanya ya kukagua ya wasafiri humo uwanjani.

Tunamuona mzungu mteja akiacha bunda la noti za dola ya Kimarekani zaidi ya alfu moja.Esther anachukua na kushindwa atazipeleka wapi.Kisha Kamata na Grace wanaingia na kuanza kuchukua zile dola Kamata akidai kuwa atampa mwenyewe pesa.Ajabu ni kuwa Kamata hakumwona yule mzungu tena.Angemjuaje?Kisha Esther na Kamata walikuwa wakisuhubiana.Esther akawaza kuwa Kamata hawezi mjua abiria huyo kwani hakumweleza wasifu wake.

 

Maudhui.

Ni adhali ya maisha ya mjini hasa kwa vijana watafutao kazi.

Tunamuona Esther akielekea Nairobi kutafuta kazi.

 

Kamata anajifanya mwema na kuchukua zile pesa na hajui anayempelekea.

 

Uaminifu

Esther anaaminika kwa kazi yake.

 

Esther amesoma na bado anataka kuendeleza masomo.

 

Shaka(kukosa uhakika)

Esther anashaka kuwa Kamata atarudisha zile pesa.

 

6 .Usasa na mabadiliko.

Zamani wanawake hawakuelimishwa lakini swala hili limeingia ambapo Kamata anampisha Esther kiti kwenye gari.

 

7.Uajibikaji.

Esther aliwajibika kazini mwake.

 

 1. Uvumilivu.

Esther anavumilia akidhani atabadilishwa zamu.

 

 1. Usaliti.

Grace anamsaliti Esther kwa kuwa na uhusiano na Kamata.

 

Wahusika.

 1. Esther.

-Ni mhusika mkuu.

-Ametoka Machakos.

-Anafanya kazi ya hoteli J.K.I.A

-Anaishi kwa mzee mwinyi.

 

 1. Mwajibikaji.

Aliajibika kwa kazi yake katika hoteli.

 1. Mshamba.

Anadanganywa kwa rahisi sana.

 

 1. Mvumilivu.

Alisubiri ili abadilishwe zamu.

 

4.Mwoga.

Hakutaka kuambia Kamata anampenda.

 

 1. Mwenye shaka.

Alishaka kwa vile pesa zitamfikia yule mzungu.

 1. Mwadilifu.

Hajiingizi katika mapenzi ya nje ya ndoa.

 1. Mwenye mapenzi ya dhati.

Anampenda Kamata.

 1. Mwaminifu.

-Alipopata zile dola alimrejeshea mteja.

-Anashawishika kwa urahisi.

 

 1. Kamata.

-Ni mfanyikazi katika uwanja wa J.K.I.A

-Ni rafikiye Grace.

-Anapenda starehe na anasa.

 1. Ndumakuwili.

-Ana uhusiano na Grace na Esther.

 1. Mlaghai.

Anamdanganya Esther.

 1. Msaliti.

Anamsaliti Esther mapenzi yake.

 1. Hana subira.

Aliona gari la Esther limekaa na kuingia kwa Grace.

 

3.Grace.

-Ni rafikiye Kamata.

-Ni mkubwa wa Esther kazini.

 

 1. Mpenda anasa.

Anaenda vilabuni kisiri na Kamata.

 1. Msaliti.

Anamsaliti Esther.

 1. Mwenye tamaa.

Anatamani bunda lile na dola la mzungu.

 1. Msiri.

Hakumweleza Esther wanaenda na nani.

 1. Mwongo.

Wana uhusiano na Kamata na kumdanganya ya Esther kuwa hawana uhusiano na Kamata.

MBINU ZA LUGHA.

 1. Maswali ya balagha.

Kuna maswali ya kuchochea hisia na ambayo hayana majibu.kwa mfano.

Esther anapokuwa kazini anawaza sana kumhusu Kamata.Anajiuliza maswali ya balagha kama Kamata kweli anamjali naye huyu pia anashughulika kutafuta pesa.

 1. Utohozi.

Baadhi ya maneno ya kizungu yametamkwa kama ya Kiswahili.km kompyuta-computer,disko-disco,blauzi-blouse.

 1. Mbinu rejeshi.

Inatumika katika (uk4) ambapo mwandishi anaturudisha nyuma katika maisha ya babake Esther.

 1. Tashhisi.

Hali ya kuvipa vitu visivyo hai sifa za vitu vyenye uhai.

 

 

 

NDOA YA SAMANI

 

 

 

 

Hadithi hii inasimuliwa katika nafsi ya kwanza.Mwandishi amechukua nafasi ya mhusika mkuu,Abu na kumtumia kusimulia.Hadithi inaanza kwa kisegere nyuma.Mbele kwa sababu msimulizi anaanza kwa sehemu inayopaswa kuwa ndiyo ya mwisho wa hadithi.

Abu anaeleza kuhusu harusi iliyokuwa ikifanyika kati yake na Amani.Mwanzoni Abu alitaka kumuoa Amali lakini kwa kuwa alikuwa maskini wazazi wa amali wakakataa.Baadaye alipata kazi ya uhamali Arabuni na kuweza kujiwekea akiba iliyomsaidia kuanzisha biashara ya uchukuzi wa abiria na kutajirika sana.

Kwa kuwa hakuwa na uhusiano wa kimapenzi na msichana yeyote,marafiki zake walimshauri amrudie Amali wake.Abu alirudi kwa akina Amani ili kumposa tena safari hii lakini wazazi wa Amali hawakumkatalia posa yake hasa kama ilivyokuwa desturi yao.Wazazi wa Amali walimshauri Amali aagize kununuliwa zawadi tele na za bei ghali na Abu.

Ikawa pia harusi sharti ifanyiwe nyumbani mwa Amali na tena iwe kukata na shoka.Siku ya arusi ilipofika kila kitu kilikuwa shwari lakini Abu alikataa kushiriki katika awa hii na hivyo basi arusi ikavunjiliwa bali.Abu alisihi kuwa Amali hakumpenda yeye bali aliyapenda mali aliyonayo sababu ya Abu kufikiri hivi ni kuwa sababu Amali alikuwa amemkataa alipokuwa maskini.Harusi iliyotarajiwa haikutendeka bali iliwaacha watu vinywa wazi.

Ndoa yapaswa kujengwa katika msingi wa mapenzi si wa mali.Mwandishi anataka kutufundisha kuwa ndoa nzuri si ya pesa.

 

1.Ndoa.

Msimulizi alimtaka Amali amwoe lakini kulikuwa na katizi kwa upande wa mvulana kwa kuwa hakuwa na pesa.Inatufunza usiolewe kwa sababu ya mali.Ndoa iwe ni maamuzi ya wenye kuoana.

2.Umaskini.

Msimulizi alikuwa ametoka kwenye familia ya kupigiwa mfano.Mwandishi anazingatia swala la umaskini lisiwe zingitiki kwa mapenzi.

2.Tamaa.

Mamake Amali alikuwa na tama ya kutajirika ndio maana alimkataa mwandishi mwanzoni.

4.Kisasi.

Msimulizi alilipiza kisasi kwa kukataa kumwoa Amali kwa vile yeye alikahaliwa mwanzoni.

5.Usaliti.

Amali alisalitiwa na msimulizi aliyemtoroka siku ya arusi.Mamake Amali alimsaliti mwandishi kwa kumkataza mwanzoni aoe Amali.Pia alimsaliti Amali kwa kumkataza aolewe na mwandishi.

6.Changamoto.

Mwandishi anapitia mambo magumu .mfano;Umaskini,kukosa kazi na pia kukataliwa na mamake Amali.

7.Bidii.

Mwandishi alienda Arabuni na kujikaza na kuwa tajiri.

8.Utajiri.

Mamake Amali anataka kutajirika.

 

1.Mwandishi.

Ni mhusika wa kiume anayopitia mambo magumu maishani.

1.Mchochole.

Kwao walikuwa maskini wa kupigiwa mfano.

2.Mwenye bidii.

Alipopata uajiri Arubani, alitia bidii na kutajirika na kuweza kujenga nyumba yake pamoja nay a wazazi wake.

3.Msaliti.

Alimsaliti Amali kwa kukosa kumuoa.

4.Mwenye kisasi.

Alikataa kumuoa Amali kwa vile alikataliwa hapo zamani kumwoa na Mamake Amali kwa kuwa hakuna na pesa.

5.Mkarimu.

Aliitikia kununua vitu ambavyo alivyopendekezwa kununulia familia yake Amali ili amuoe.Pia aliwatafutia ndugu zake kazi huko Arabuni.

2.Amali.

Msichana aliyetakiwa kuolewa na msimulizi.

1.Mtawa.

Anakaa kwao nyumbani na kutojishughulisha kwenda kufanya mapenzi kiholela.

2.Mtiifu.

Anawatii wazazi wake na pia dini yake.

3.Mrembo.

Wengi walimtaka kwa sababu ya urembo mwandishi aliyesoma.

4.Mtamaduni.

Alifuata mambo ya kitamaduni.

3.Wazazi wa Amali.

(i)Mamake.

1.Mwenye tamaa.

Anaitisha mahali ya bintiye ili atajirike.

2.Mwenye ubinafsi.

Anajiitishia vitu vyake pekee kama mahari ili Amali aolewe.

Mtindo wa lugha.

Ametumia misemo .kwa mfano;

Kupata jiko-kuoa

Walalahai-tajiri

Walalahoi-maskini

Maskini hohehahe-umaskini

 

 

 

MIZIZI NA MATAWI

 

Hadithi hii inatusimulia kisa cha mvulana mmoja kwa jina lake Sudi.Alilelewa na mama tajiri aliyemsomesha hadi chuo kikuu na mwishowe akaajiriwa.Alizoea kuuliza kama alikuwa na babake mzazi tangu utotoni akajulizwa kuwa babake mzazi ni Abdalla lakini hajawahi muona.

Siku moja alimuuliza mamake aliyetengeneza hadithi ya uongo kuwa Abdalla alimkimbia akiwa bado hajamzaa Sudi.Jioni moja Sudi akitoka stareheni zake alikutana na mwanamke mmoja aliyemwomba usaidizi.Alimpeleka hadi kwao na kumwajiri kama yaya.Bibi huyu alimsimulia Bi.Mkubwa jinsi alivyomtupa mtoto kwenye pupa la taka kwa kukosa uwezo wa kumlea.

Baadaye Bi.Mkubwa alimweleza Sudi kuwa mamake mzazi ni yule mfanyikazi wake na kuomba wasameheane.

Hadithi hii inatufunza kuwa hata mtu akipotelewa na waliokaribu naye ama wakose kumsaidia bado anaweza kuendelea na kufaulu maishani.

1.Mapenzi.

Sudi alipendwa na wasichana wawili Radhia na Waridi.Wasichana wengine pia walimpenda Sudi kwa utanashati wake.

2.Ukatili.

Bi.Kudura alifanya ukatili kwa kumtupa mwanawe kwenye pipa la takataka.Alijua hili lilikuwa kama kuua lakini hakujali.

3.Majuto.

Bi.Kudura anajuta kwa kumtupa mwanawe na baadaye hakuweza kupata mtoto aliomba Mola amsamehe.

4.Uana haramu/malezi.

Sudi hakumjua babake jambo lililomsumbua sana kimawazo.

Alimuomba mamake amwambie ukweli lakini alimdanganya.

5.Elimu.

Licha ya kuwa mwanaharamu,Sudi alisomeshwa na mamake hadi kiwango cha juu hadi akawa daktari.

6.Anasa.

Sudi alipokuwa ulaya alihudhuria sherehe iliyokuwa ya kukata na shoka ambayo ilikuwa ni sikukuu ya pasaka.Kulikuwa na muziki na wanawake wengi walitaka kucheza na Sudi.Pia alimpeleka mpenziwe Radhia kustarehe huko.

1.Sudi Abdalla.

(a)Mtana shati.

Ni kijana aliyependa usafi sana kwani tunamwona akijikwatua alipokuwa akijiandaa kwenda karamuni.

(b)Mkarimu.

Mara kwa mara alimpata Bi.Kudura njiani na hakumpita .Alimpa msaada aliotaka.

(c)Mwenye heshima.

Aliwaheshimu mamake na Bi.Kudura .Licha ya kuwa Bi.Kudura alikuwa maskini mwombaji,Sudi alimwita kwa majina ya heshima.Pia hakuwahi kumtuma amletee chochote.

(d)Mwenye utu.

Kutokana na utu wakealimsaidia Bi.Kudura.Alimwonea huruma alipompata njiani karibu na makaburi.

(e)Anapenda anasa.

Anapenda kuhudhuria karamuni na sherehe na mpenziwe Radhia.

(f)Mwenye mapenzi ya dhati.

Alimpenda sana mamake na Radhia mpenziwe na kufanya uchumba naye.

 

2.Bi Mkubwa.

Huyu ndiye aliyemwokoa Sudi alipotupwa kwenye pipa la takataka na mamake mzazi.Alimlea kama mwanaye.

Sifa zake.

1.Ni mwongo.

Alimdanganya Sudi kuwa yeye ndiye mamake mzazi na kuwa babake alikuwa akiitwa Abdalla lakini alikufa na kumwachia mamake ulezi.

2.Ni mkarimu.

Bi.Kudura alipopelekwa kwake alikubali kukaa naye na hata akampa vitu alivyoagizwa na Sudi.

3.Ni msiri.

Aliweza kuiweka siri juu ya asili ya Sudi kwa muda mrefu tangu Sudi akiwa mtoto.

4.Mwenye mapenzi ya dhati.

Bi Mkubwa alimpenda Sudi na kumlea kama mwanaye.

5.Msamehevu.

Alimsamehe Bi.Kudura naye akasamehewa na Sudi.

 

3.Bi.Kudura.

Huyu ndiye aliyemzaa Sudi nje ya ndoa na kumtupa kwenye pipa la takataka kwa sababu aliona aibu.

Sifa zake.

(a)Ni mkatili.

Alifanya ukatili kwa kumtupa mtoto mchanga kwani hakujua kama angeokotwa na mtu au angeliwa na mnyama.

(b)Ni mnyenyekevu.

Kwa sababu ya hali yake ya umaskini alinyenyekea ili asaidiwe.

(c)Ni mcha mungu.

Alijua kuwa tendo la kumtupa mwanawe ilikuwa dhambi kwa mungu.

 

MBINU ZA SANAA NA LUGHA.

1.Taharuki.

Sudi alikuwa na hamu ya kumjua babake mzazi.Naye mamake alimweka na taharuki kwa muda mrefu.

2.Methali

-Mungu akikupa kilema hukupa na mwendo.Sudi alitaka mamake amwambie ukweli ndipo ajue jinsi ya kuishi na ukweli huo.

-……yaliyopita huwa yamepita.Sudi alitaka kuyasahau maisha ya anasa aliyoishi alipokuwa ulaya.

-Kuvyaa kupona.Mwanamke anapopata mtoto,mtoto huyo atakuja kumfaa baadaye akiwa mkubwa.

-Damu ni nzito kuliko maji.Bi.Kudura aliongozwa na kudura hadi ilipo damu yake na kumpata mwanawe Sudi.

3.Misemo.

-Kata tama-kosa matumaini.

-Tulia kama maji ya mtungi-tulia sana.

-Piga gari moto-Gurumisha gari.

-Walikuwa hawajijui hawajitambui-hawajiwezi.

-Piga moyo konde-Amua kufanya jambo.

4.Maswali ya balagha.

-Furaha yangu itoke wapi tena?

-Kuna ukatili gani zaidi ya huo?

5.Kuchanganya ndimi.

Kwa mfano:Handsome,Tea breeze,Royal palm.

6.Uzungumzi nafsia.

Sudi alijisemea mwenyewe anaposema.’Kumbe ni kweli wanavyoniita’Sudi alisaini kimoyomoyo.

7.Tashhisi.

Gari unahaishwa tunapoambiwa kuwa Sudi alipiga gari lake moto na taratibu likatambaa na kuanza masafa kuelekea lilikokusudiwa.

8.Jazanda.

Kwa Sudi maneno haya yalikuwa msumeno unaokeketa kwa maumivu makti.

9.Tashbihi.

…..lakini ulimi wangu mzito kama nanga.

10.Mbinu rejeshi.

Sudi anaturejesha nyuma huko ulaya alipokuwa akisomea na kutuonyesha jinsi maisha yalivyokuwa.

11.Sadfa.

Kukutana kwa Sudi na Bi. Kudura ilikuwa sadfa kwani hakutarajiwa.

12.Utohozi.

Hoteli-hotel

Bia-beer

Muziki-music

Benki-bank

Densi-dance

13.Nidaa.

Sudi alikuwa akitabasamu-tabasamu ya fahari kwa uzuri wake.

Alifariki ghafla na kuniacha na mimba yako,tena changa!

Ikawa kama mtu aliyefundua tandu akafundika nge.

Naam,watu walikuwa wawiliwawili…ndume na mke!

Alimrudi kila mmoja alikuwa na ulimwengu wake.

Inanikumbusha kauli ya wahenga …kuvyaa kupona!

Aa vile nao na umetulia! Hapo kabsa!

Facebook

Get the Facebook Likebox Slider Pro for WordPress
Powered by "To Do List Member"